Geti la kuingilia kwenye ghala lililoteketea kwa moto |
Gari la polisi maarufu kwa washa washa likisaidia kuzima moto tofauti na ilivyozoeleka kuwa linatumika katika kuondoa vurugu |
Vikosi vya uokoaji vikiendelea na zoezi la kuzima moto |
Baadhi ya bidhaa zikiwa zimesambaa chini katika ajali ya moto |
GHALA la kuhifadhia bidhaa
mbali mbali za vyakula ukiwemo unga na mafuta ya kupikia limeteketea kwa moto
eneo la Forest jijini Mbeya.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa
tukio hilo walisema moto huo ulianza kuwaka majira ya asubuhi leo na kuteketeza
baadhi ya vitu kabla ya Jeshi la zimamoto na uokoaji hawafika.
Mashuhuda hao ambao hawakutaka
kutaja majina yao walisema ghala hilo ambalo getini kumeandikwa jina la Azania haijafahamika
chanzo cha moto huo na kuongeza kuwa waliona moshi mkubwa ukitoka katika eneo hilo.
Walisema taarifa za awali
zinadai kuwa mmiliki wa ghala hilo ndiyo yule Yule aliyewahi kuunguliwa na
ghala lingine kipindi cha nyuma karibu na uwanja wa ndege wa zamani(Airport).
Hadi tunaingia mtamboni hakuna
taarifa iliyotolewa juu ya hasara iliyopatikana katika ajali hiyo hata
majeruhi.
No comments:
Post a Comment