Mshindi wa Airtel Mkwanjika, Ismail Mwaswale akipewa maelezo kabla ya kuingia kwenye boksi la kuokota fedha katika shindano la kwangua ushinde |
Mshindi wa Airtel Mkwanjika, Ismail Mwaswale akiwa kwenye boksi la kuokota fedha katika shindano la kwangua ushinde akiendelea kujikusanyia mapesa. |
Mshindi wa Airtel Mkwanjika, Ismail Mwaswale akishuhudia fedha alizookota zikihesabiwa katika shindano la kwangua ushinde |
Iddi Yusufu akiendelea kuokota fedha katika boksi kwenye shindano la kwangua ushinde na Airtel Mkwanjika |
Mshindi Jotham Mwainyekule akijaribu bahati yake kama anaweza kuokota fedha zote ambazo ni shilingi Milioni Moja anazopaswa kuziokota kwa muda wa sekunde 60 |
Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Mbeya wakishuhudia shindano la Kwangua ushinde la Airtel Mkwanjika |
Mshereshaji wa Airtel Mkwanjika akitoa maelekezo kabla ya kuanza kwa shindano kwa washindi kuokota fedha |
Mmoja wa Watumishi wa Airtel akionesha mfano jinsi ya kushiriki zoezi la kuokota fedha linavyopaswa kufanyika |
PROMOSHENI inayoendeshwa na
Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel inayojulikana kwa jina la Kwangua ushinde
na Airtel Mkwanjika imetua katika Mikoa ya Nyanda za Juu kusini ambapo washindi
nane wamepatikana na kujizolea fedha taslimu.
Zoezi la kuwapatia zawadi
washindi hao lilifanyika jana katika ofisi za Kanda za Airtel zilizopo Uhindini
Jijini Mbeya na kushuhudiwa na wakazi wa Jiji hilo kutokana na zoezi hilo
kufanyika katika maeneo ya wazi.
Meneja Mauzo wa Airtel Kanda ya
Nyanda za juu kusini, Straton Mushi alisema tangu shindano hilo lianze mwezi
Disemba mwaka jana nchi nzima wateja wengi wamejitokeza na kujizolea fedha
lukuki ambazo zimekuwa zikiwasaidia katika kuboresha hali yao ya kiuchumi kwa
kuongeza vipato vyao.
Alisema hakuna masharti yoyote
ya mteja kujishindia bali anachopaswa ni kununua vocha na kuikwangua kasha kuijaza
kwenye simu yake ya Airtel anakuwa ameingia moja kwa moja kwenye shindano
ambapo baada ya kuchaguliwa huingizwa kwenye boksi maalum lenye fedha taslimu
shilingi Milioni moja ambazo hupulizwa na upepo hivyo kasi ya mteja kuokota
fedha ndizo zinakuwa zawadi yake.
Aliwataja washindi walioshiriki
kujiokoteza fedha kwa Kanda kuwa ni pamoja na Ismail Mwaswale (Sumbawanga)
ambaye kwenye boksi alijiokotea jumla ya shilingi 920,000 kwa muda wa sekunde
sitini akifuatiwa na Iddi Yusufu (Iringa) aliyeokota shilingi 750,000 na Jotham
Mwainyekule mkazi wa Mbozi aliyepata shilingi 730,000/=.
Aliwataja washindi wengine kuwa
ni Kazembe Salamanda Mkazi wa Ruvuma, Onesmo Lubaga mkazi wa Iringa, Tonny
Moris Mkazi wa Mbeya, Bahati Muhawala mkazi wa Mbeya na Thomas Baraka mkazi wa
Rukwa ambao viwango vyao havikujulikana mara moja.
Wakizungumza baada ya kumalisha
shindano hilo washindi hao walitoa wito kwa watanzania kuiamini Airtel na
kuitumia kwa kuwa huduma zao ni za kweli na uhakika tofauti na madai ya wengi
kuwa promosheni hizo ni danganya toto.
Ismaila Mwaswale(43)Mkazi wa
Sumbawanga na mfanyabiashara mdogo alisema baada ya kupigiwa simu kwamba
ameshinda hakuamini hadi pale alipotumiwa nauli ya kuja kushiriki zoezi hilo
mkoani Mbeya.
Alisema fedha alizopata
zitamsaidia kuongeza mtaji wa biashara yake ambayo imekuwa ikisuasua kutokana
na mtaji mdogo huku fedha zingine akizielekeza kulipia karo za watoto wanaosoma
shule binafsi.
Iddi Yusuph (26) mkazi wa
Iringa alisema ni vema Watanzania na wateja wa Airtel wakaamini kuwa kichezo
hiyo ipo na inafanyika kweli wala sio utapeli na haifanyiki kwa kujuana na
watumishi wa airtel kwani yeye mwenyewe ameshinda pasipo kutoa chochote wala
kujuana na mtumishi yeyote.
Baadhi ya mashuhuda wa
mashindano hayo walisema ni jambo zuri linalofanywa na Kampuni ya Airtel kwa
kuweka mashindano ya wazi ambapo kila mtu anaona namna mshiriki anavyohangaika
kuokjota fedha kutoka kwenye boksi na kwamba hali hilyo huonesha kuwa hakuna
upendeleo.
No comments:
Post a Comment