Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, December 14, 2015

VITUO VYA KULELEA WATOTO YATIMA VITAZAMWE UPYA, SERIKALI IVIKUMBUKE.

Meneja wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Nuru Orphance Centre, Amanda Fihavango akiwa mbele ya vitu vilivyotolewa kama msaada na msamaria mwema kutoka nchini Marekani.

Meneja wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Nuru Orphance Centre, Amanda Fihavango akijadiliana jambo na mwakilisha wa msamaria kutoka Marekani Vida Katamba, Daynes Macha ambaye alipeleka msaada wa vitu mbali mbali kwa niaba yake.

Dynes Macha akiwa amemshika mtoto mchanga zaidi kati ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Nuru

Dynes Macha akiwakabidhi watoto msaada wa vitu mbali mbali kwa niaba ya rafiki yake anayeishi nchini Marekani  Vida Katamba

Watoto wa wanaolelewa katika kituo cha Nuru wakifurahia msaada wa vitu mbali mbali baada ya kukabidhiwa, wengine kwenye picha ya pamoja ni Joseph Mwaisango wa pili kulia.

Meneja wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Nuru Orphance Centre, Amanda Fihavango akipongezana na  mwakilisha wa msamaria kutoka Marekani Vida Katamba, Daynes Macha ambaye alipeleka msaada wa vitu mbali mbali kwa niaba yake.

Watoto wakifurahia msaada

Mmoja wa Walezi na wahudumu wa kituo cha Nuru akigawa juisi kwa Watoto

Joseph Mwaisango ambaye ni mmiliki wa Blog ya Mbeya yetu akifurahia jambo na watoto wanaolelewa katika kituo cha Watoto Yatima cha Nuru.
SERIKALI ya Awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Magufuli imeombwa kuviangalia kwa ukaribu vituo vya kulelea watoto yatima kwa kuvipatia ruzuku ili viweze kujiendesha vyenyewe tofauti na hivi sasa vinategemea misaada kutoka kwa wasamaria wema.
Rai hiyo ilitolewa na Meneja wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Nuru Orphans Centre, Amanda Fihavango kilichopo Uyole jijini Mbeya alipokuwa akipokea msaada kutoka kwa wasamalia wema ambao ni Watanzania wanaoishi nchini Marekani.
Meneja huyo alisema Kituo hicho chenye watoto 26 kati yao wavulana  10 na wasichana  16 wenye umri kuanzia wiki moja hadi miaka 10 wanakabiliwa na ugumu wa uendeshaji wa shughuli za kila siku ikiwa ni pamoja na vyakula pamoja na fedha za kuwalipa wahudumu wanaokaa na watoto hao.
Alisema watoto waliopo kituoni hapo mara nyingi hupelekwa baada ya kutelekezwa na mama zao mara baada ya kujifungua hali inayopelekea kuwa waangalifu katika kuokoa maisha yao kwani wengine hupokelewa wakiwa wamejeruhiwa kutokana na kutupwa.
Meneja huyo aliongeza kuwa baadhi ya watoto hupelekwa na baba zao baada ya mama kufariki dunia akiwa anajifungua hivyo humsaidia baba kulea ambapo huruhusiwa kumchukua baada ya kukua na kufikisha miaka miwili.
Aidha alitoa wito kwa wazazi hususani vijana kuacha tabia ya kuwapeleka watoto wachanga kwa bibi zao kwani asilimia kubwa wanakosa malezi bora kutokana na walezi hao kuwa na hali mbaya ya kiuchumi hivyo kushindwa kutoa huduma stahiki kwa motto mchanga na badala yake wawe na utaratibu wa kuwapeleka kwenye vituo vinavyotambulika.
Alisema changamoto kubwa inayokikabili kituo hicho mbali na ukosefu wa fedha ni uhaba wa viatu na mavazi kwa watoto wakubwa kuanzia miaka mitano hadi kumi kutokana na gharama kubwa ya nguo zao tofauti na watoto wachanga ambao hupatiwa misaada kiurahisi.
Alisema changamoto nyingine ni ukosefu wa uzio kukizunguka kituo hicho kwani huhatarisha maisha ya watoto ikiwa ni pamoja na kuibiwa vitu, kushindwa kuweka vifaa vya kuchezea na kushindwa kuwadhibiti watoto wengine kutoroka kutokana na kuwa watundu kupita kiasi.
Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo kwa niaba ya Rafiki yake ambaye anaishi Marekani, Vida Katamba, Dynes Macha alisema wametoa msaada huo kama ishara ya kusherekea sikukuu za Krismas na Mwaka mpya pamoja na watoto yatima.
Macha alivitaja vitu vilivyopelekwa kuwa ni pamoja na Unga wa ngano kilo 25, unga wa sembe kilo 25, mafuta ya kupikia lita 10, sukari kilo 20,sabuni ya unga kilo 15,sabuni ya mche boksi moja,mchele kilo 40,chumvi ndogo katoni moja,mafuta ya kupaka dazani moja na nusu,sabuni za kuogea dazani 2, juisi dazani mbili na pipi kopo moja.

1 comment:

Anonymous said...

Asante sana Josephy I know bila wewe nisingeweza thanx sana na MUNGU AKUJALIE BRO

thanx u make ma bday go like what I wa s plan thanx sana