Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa maagizo ya Rais. |
Afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Mbeya, Stellah Kategile akisoma taarifa ya utekelezaji wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani kwa Mkoa wa Mbeya |
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akimkabidhi boksi la dawa kwa ajili ya watu wanaoishi na maambukizi ya VVU Mganga mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dk. Seif Mhina kwa ajili ya kuzisambaza kwa watumiaji. |
Baadhi ya madawa na vifaa mbali mbali vilivyonunuliwa kutokana na gharama za maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani zilizokuwa zifanyike kimkoa Wilaya ya Mbarali zikiwa kuokolewa |
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya |
Akizungumza katika mkutano na waandishi
wa habari uliofanyika ofisini kwake, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro
alisema katika maadhimisho yaliyofanyika Disemba mosi mwaka huu kuna shughuli
nyingi zimeshafanyika ikiwa ni pamoja na ununzi wa madawa, utoaji wa elimu na
shughuli za kijamii.
Kandoro alisema jumla ya madawa
yenye thamani ya shilingi Milion 3,550,000 yamenunuliwa na kukabidhiwa kwa
Mganga mkuu wa Mkoa ambaye atasambaza katika Zahanati, Vituo vya Afya na
Mahospitali yanayotoa huduma.
Alisema maandalizi ya
maadhimisho hayo ambayo yalikuwa yafanyike Wilayani Mbarali kimkoa yalianza
Novemba 13 mwaka huu kabla ya maagizo ya Rais kutolewa ambapo wadau zaidi ya 50
walijitokeza na kuchangia fedha pamoja na vifaa mbali mbali vyenye thamani ya
shilingi Milioni 32.
Alisema vifaa vilivyotolewa
kuwa ni pamoja na Mipira, sare za mpira, mafuta ya gari, vipeperushi,Kondomu,
vikombe, kofia, T shirt, Ndoo na Kanga ambavyo vyote watapewa walingwa ambao ni
Watu wanaoishi na Maambukizi ya Virusi vya ukimwi.
Alisema shughuli zilizofanyika
ni pamoja na kuendesha midahalo ya wazi katika jamii kuhusu kujikinga na
maambukizi mapya ya Ukimwi katika Kata za Igulusi, Chimala, Mapogoro,Rujewa na
Ubaruku katika Wilaya ya Mbarali.
Aliongeza kuwa shughuli zingine
ni pamoja na kuendesha mashindano mbali mbali ya mpira wa miguu, kutoa mafunzo
kwa waelimisha rika, Semina, Ushauri nasaha na upimaji pamoja na kutembelea
klabu za watoto wanaoishi na VVU.
Kuhusu maadhimisho ya sherehe
ya miaka 54 ya Tanzania Bara Kandoro alisema Mkoa wa Mbeya umeanza kutekeleza
agizo la Rais la kuitumia siku hiyo kufanya usafi ambapo katika kikao cha
viongozi wa Wilaya zote walikubaliana kuanza utekelezaji Disema 2 mwaka huu kwa
kila Halmashauri kutenga siku ya kufanya usafi.
Alisema mbali na kuanza tarehe
mbili pia waliazimia kutenga siku ya Jumamosi ya kila wiki kuwa ni siku ya
usafi ili kujenga tabia ya wananchi kuuchukia uchafu na kupenda usafi ili zoezi
hilo kuwa endelevu.
Alisema siku ya kilele ya
Disemba 9 kila mwananchi kuanzia ngazi ya Kaya hadi Halmashauri bila kujali
nafasi aliyonayo anapaswa kujitokeza kufanya usafi katika maeneo
yanayowazunguka kwa kuhakikisha mifereji na mitaro inazibuliwa.
Alisema kuna changamoto ya
vifaa vya kuzibulia mifereji pamoja na usombaji wa taka ambapo ameziagiza
Halmashauri zote kuhakikisha wanapata vifaa hivyo ikiwa ni kwa kukodi ama
kuazima ili mradi zoezi lifanyika kwa kiwango kizuri.
No comments:
Post a Comment