Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, December 1, 2015

WACHINA KIZIMBANI KWA KOSA LA UHUJUMU UCHUMI BAADA YA KUKUTWA NA PEMBE ZA FARU

Washtakiwa wa uhujumu uchumi wakiwa kizimbani kutoka kulia ni Song Lei, Xiao Shaodan, Chen Jianlin na Hu Liang.

Wakili anayewatetea Washtakiwa wa Uhujumu Uchumi, Ladislaus Lwekaza akizungumza na wachina kabla ya kuanza kusikiliza kesi yao.

Waendesha Mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa (kushoto) na Wankyo Saimon wakibadilishana mawazo wakisubiri kesi kuanza kusikilizwa

Lwekaza akimsikiliza Mkalimani wa lugha ya kichina Manfred Lyoto alipokuwa akizungumza na wachina

Maafisa wa Polisi na Forodha wakionesha Pembe za Faru ambazo walikamatwa nazo raia wa China

Wachina wakipanda kwenye karandinga la Polisi tayari kurudishwa Rumande baada ya kesi yao kuahirishwa


Wachina wakiingia kwenye Chumba cha Mahakama.
 
RAIA wanne wa China juzi walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya wakituhumiwa kwa makosa matatu ikiwemo kupanga na kutekeleza njama za uingizaji wa pembe za faru nchini bila kibali cha Serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa.
 
Washtakiwa hao walisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi, Michael Mteite na mwendesha mashtaka wa Serikali Archiles Mulisa ambaye aliwataja washtakiwa kuwa ni Song Lei, Xiao Shaodan, Chen Jianlin na Hu Liang.
 
Mulisa alidai mahakamani hapo kuwa watuhumiwa walikamatwa eneo la mpakani Kasumulu wilayani Kyela wakiwa na vipande 11 vya pembe za Faru vyenye thamanbi ya shilingi 902,880,000 wakitoka navyo nchini Malawi kinyume cha sheria kifungu cha 5 cha mwaka 2009 cha sheria ya wanyama pori.
 
Mulisa aliyataja makosa mengine katika kesi namba 6 ya mwaka 2015 kuwa ni kujihusisha na nyara za serikali kinyume cha sheria za wanyamapori na kuhujumu uchumi na kosa linguine ni kumiliki nyara za serikali bila uhalali na kinyume cha sheria ya uhifadhi ya wanyama pori.
 
Washtakiwa wote walikana mashtaka ambapo upande wa Mashtaka ulisema unao mashahidi watano na upelelezi umekamilika na wapo tayari kuendelea na kesi huku upande wa utetezi ukitetewa na Wakili Ladislaus Lwekaza ukiwa hauna kipingamizi.
 
Hakimu Mkazi Mteite aliahirisha Kesi hadi siku inayofuata kwa ajili ya kuendelea kusikiliza mashahidi watakaoletwa na upande wa Jamhuri.
 

No comments: