Wanahabari wa Mkoa wa Mbeya wakichukua kumbukumbu mbali mbali katika maporomoko ya Kaporogwe yaliyoko Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya. |
Wanahabari wa Mkoa wa Mbeya wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kushuka kwenye maporomoko ya Kaporogwe. |
Wanahabari wa Mkoa wa Mbeya wakielekea sehemu ya Maporomoko |
Waandishi wa Habari mkoani Mbeya wakiwa ndani ya Pango katika maporomoko ya Kaporogwe ambapo sehemu hiyo haiguswi na maji ya mvua ikinyesha. |
Baadhi ya wanahabari wakipunzika katika mapango yaliyoko katika maporomoko ya Kaporogwe |
Kumbukumbu mbali mbali zikichukuliwa |
Wanahabari wakiendelea kuhojiana baada ya kuridhika na kile walichokiona katika ziara yao. |
WANANCHI
wametakiwa kujitokeza kujifunza kutokana na maeneo ya vivutio vya utalii
vilivyopo katika maeneo yao ili kukuza uchumi wa ndani.
Hayo
yalibainishwa mwishoni mwa wiki na Wanahabari mkoani Mbeya kupitia chama chao
cha Mbeya Press Club(MBPC) walipotembelea maporomoko ya maji ya Kapologwe
yaliyopo katika kijiji cha Bugoba kata ya Kisondela wilayani hapa.
Wanahabari
walifika kwenye maporomoko hayo ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya kimafunzo
waliyoifanya katika vijiji mbalimbali
vya kata ya Kisondelo lengo likiwa ni kujifunza juu ya maisha ya wakazi wa
vijiji hivyo.
Wakizungumza
mara baada ya kutembelea maporomoko ya Kaporogwe,wanahabari waliokuwa kwenye
ziara hiyo walisema maporomoko hayo ni moja ya vivutio vya utalii vinavyopaswa
kutangazwa zaidi ili kuwezesha watu kutoka ndani na nje ya nchi kuyatambua.
Mwenyekiti
wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mbeya(MBPC) Modestus Nkulu alisema
maporomoko hayo ni miongoni mwa hazina zenye manufaa makubwa iwapo zitatangazwa
na kuhamasisha jamii kuyatambelea.
“Maporomoko
kama haya ni hazina tosha kiutalii.Wengi wetu hatukuwahi amini kuwa ipo siku
tutakutana na mambo ya ajabu kama haya.Uwepo wa pango kubwa kama tuliloliona na
pia maji yanayotiririka hapa ni mambo ya ajabu sana.Nawasihi watanzania wengine
tuimarishe utalii wa ndani kwa kutembelea kivutio hiki” alisisitiza Nkulu.
Alisema
kwa wakazi waishio mkoani Mbeya hawapaswi kusimuliwa juu ya uwepo wa maporomoko
haya ya ajabu mkoani kwao hivyo wana fursa nzuri ya kufika na kujionea ili
wanaposafiri kwenda mikoa mingine wakiulizwa na wenzao huko wawe na majibu
sahihi.
Nao
wanahabari Joachim Nyambo na Amina Said walisema ziara hiyo imekuwa na
mafanikio makubwa kimafunzo kutokana na mambo waliyoyashuhudia wakisema hiyo
itakuwa chanchu ya kutangazwa kwa vivutio vya utalii.
Walishauri
wadau mbalimbali mkoani hapa kuona umuhimu wa kuwawezesha wanahabari kuvifikia
vivutio vya utalii vilivyopo ndani ya mkoa wao.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment