Afisa uhusiano wa Mamlaka Maji safi na usafi wa Mazingira Jiji la Mbeya Neema Stantoni. |
MAMLAKA ya Maji safi na usafi wa mazingira Jiji la Mbeya(MBEYA
UWSA)imewataka wateja wake kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho
kuna tatizo kubwa la maji lililosababishwa na ukosefu wa umeme.
Wito huo ulitolewa na Afisa uhusiano wa Mamlaka hiyo, Neema Stantoni, alipokuwa akizungumza kuhusiana na tatizo la maji linalolikabili Jiji la Mbeya kwa kipindi cha wiki mbili sasa.
Stantoni alisema pamoja na wananchi kupata athari kubwa lakini pia mamlaka onapata hasara kwani malipo ya mwisho wa mwezi yatapungua kwa kiwango kikubwa kutokana na wateja webgi kutokuwa na maji kwa muda mrefu.
Alisema tatizo la maji limetokana na kuwepo kwa katizo la umeme hivyo kushindwa kusukuma maji kutoka kwenye chanzo hadi kwenye matanki ya kuhifadhia hivyo kusababisha baadhi ya maeneo kukosa kabisa maji hususani maeneo ya miinuko.
Alisema hivi sasa umeme unaopatikana hautoshelezi kuweza kujaza matanki yote yanayoweza kutosheleza mahitaji ya Jiji la Mbeya ambalo hutumia lita za ujazo 38,000 kwa siku hadi kufikia lita 43000 kwa kipindi cha kiangazi cha mwezi Agosti,Septemba na Oktoba.
Alisema kutokana na tatizo ka umeme hivi sasa maji yanayopatikana na lita za ujazo 18,000 na kuongeza kuwa umeme hupatikana kwa masaa 6 na kushuka chini hivyo kushindwa kujaza matanki kama inavyotakiwa.
Aliongeza kuwa tatizo hutokea katika baadhi ya maeneo ambayo hupata maji kutokana na kuwa sehemu za miteremko hivyo huwezesha maji kushuka kirahisi hata bila kutegemea nishati ya umeme.
“Wananchi wengi wanaandamana wakitaka maji na tukiwaambia tatizo ni umeme wanakuwa wakali kutokana na baadhi maji kutoka lakini hili linatokana na jografia mfano maji yakitoka chanzo cha Ivumwe kwenda Iyela huenda kwa mseleleko lakini hayawezi kuingia kwenye tanki hadi umeme uwepo” alifafanua Stantoni.
Alisema Mamlaka hiyo inamitambo zaodi ya 10 ambayo hutegemea nishati ya umeme kuweza kusukuma maji hadi kwenye matanki ambapo kama umeme ukiwepo kwa masaa 24 tatizo hilo linaweza kuisha kwa kiwango kikubwa.
Alisema hivi sasa wako kwenye mazungumzo na shirika la Umeme ili kutoa vipaumbele katika maeneo hayo kwani shirika pia linaweza kupata hasara kwa sababu Mamlaka pekee hulipa zaidi ya shilingi Milioni 80 kwa mwezi kwa matumizi ua umeme wa mitambo.
Aliyataja maeneo ambayo yanahitaji zaidi umeme kuwa ni pamoja na chanzo cha Swaya,Nsalaga, Iyela,Nzovwe,Nelotia,Veta,Kadeghe,Iduda,Imeta, Sisimba,Nsoho,Iwambi na Mwatezi.

No comments:
Post a Comment