Walioondolewa
katika nyumba za Kanisa ni pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kanisa hilo
Nosigwe Buya aliyekuwa akiishi Jacaranda,Jamson Mwiligumo aliyekuwa akiishi
Meta,Edward Chilale aliyekuwa akiishi Ushirika wa Bethelehemu Mama John,Nehemia
Mwalupembe aliyekuwa Ushirika wa Panda Hill Songwe na Joseph Mwakyoma aliyekuwa
akiishi Itiji Jijini Mbeya.
Mweyekiti wa
Baraza la Ardhi amesema kuwa maamuzi hayo ni madogo katika shauri mama
linalosikilizwa katika Baraza hilo shauri ambalo lilifikishwa mapema mwaka jana
na Kanisa likiwataka wahame baada ya kuwaachisha kazi.
Aidha
Mwenyekiti wa Baraza amesema shauri mama litaendelea kusikizwa Barazani hapo
Novemba 11 mwaka huu na kwamba kwa sasa Wachungaji hao hawapaswi kuwepo katika
nyumba za Kanisa wakati shauri likiendelea kusikilizwa.
Mgogoro huo
wa Kanisa umedumu kwa zaidi ya miaka miwili ambapo Wachungaji hao wamekuwa na
Mgogoro na Mwajiri wao ambaye ni Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini
Magharibi.
Baadhi ya
madai ni pamoja na kupinga kuenguliwa Uenyekiti Mchungaji Nosigwe Buya na kutaka kuitishwa kwa Sinodi ya
dharula ili kumrejesha kazini Mwenyekiti huyo baada ya tuhuma za ubadhilifu wa
fedha za Kanisa.
No comments:
Post a Comment