Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Mbeya mjini, Sambwee Shitambala akizungumza katika mkutano wa kampeni kata ya Ghana |
Meneja Kampeni wa Mgombea Ubunge Jimbo la Mbeya mjini kwa tiketi ya CCM, Charles Mwakipesile akimnadi mgombea Sambwee Shitambala |
Katibu wa Siasa, Itikadi na Uenezi wa CCM Mbeya mjini, Philimon Mng'ong'o akiwaongoza wafuasi na wapenzi wa Chama hicho kuimba nyyimbo za hamasa |
Baadhi ya wanachama wa CCM waliojitokeza kusikiliza sera za mgombea ubunge |
Tukio hilo lilitokea baada ya Sugu akiwa na msafara wa vijana wa bodaboda wakipita eneo anbalo Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM, Sambwee Shitambala alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni katika kata ya Ghana jijini Mbeya.
Sugu na msafara huo walifika eneo hilo kwa kile kilichodaiwa walikuwa wakielekea Kata ya Nsoho majira ta saa kumi na nusu jioni ambapo alizuiliwa na wafuasi wa CCM ambao walimwamuru kupita njia nyingine lakini alikaidi na kulazimisha kupita kwa nguvu ndipo vurugu zilipoibuka na kuvunjwa kwa vioo vua gari ya mbunge huyo.
Hata hivyo baada ya kufanikiwa kupenya Mbilinyi alirudi tena baada ya saa moja akiwa amebadilisha gari huku akiwa ameongeza idadi ya vijana wa bodaboda ambao walikuwa wameshika silaha mbali mbali yakiwemo marungu ambao makada wa CCM baada ya kuona hivyo waliamua kuwapisha kuendelea na safari yao.
Baadhi ya wananchi waliokuwepo eneo la tukio walisema alichokifanya Sugu ni ukorofi kwani alikuwa ameshamaliza mkutano wake wa Kampeni katika Kata ya Nsoho hivyo kitendo cha kurudi kulikuwa na ishara ya vurugu na kwamba njia za kuelekea eneo hilo zipo zaidi ya mbili hivyo alikusudia kufanya fujo.
Akizungumzia sakata hilo, Katibu wa Siasa, Itikadi na Uenezi wa CCM, Wilaya ya Mbeya Mjini, Philimon Mg’ong’o alisema kwa sasa hawako tayari kuvumilia vitendo vya vurugu ambavyo Chama chake kimekuwa kikitendewa na vijana wa Chadema wakiongozwa na mgombea wao.
Naye Meneja wa kampeni wa Ngombea Mbunge wa CCM, Charles Mwakipesile alisema Sugu pamoja na wafusi wake wa Chadema wamepanga kuharibu ratiba ya CCM ya kufanya kampeni jambo ambalo hawatakubali kufayiwa hivyo na badala yake wataendelea na kampeni na hawako tayari kwajibu kwa sasa bali adhabu yao ni Oktoba 25 mwaka huu.
Aliongeza kuwa hata mabadiliko wanayoyahubiri kila siku ni kuwaondolea amani wakazi wa Mbeya na kuwapeleka kwenye vurugu ambazo dalili zake zimeanza kuonekana kabla ya uchaguzi mkuu na kwamba wakazi wa Jiji la Mbeya wanayonafasi ya kuchagua amani ama vurugu.
Kwa upande wake Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbeya mjini kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM), Sambwee Shitambala, alisema hizo vurugu zilizofanywa na Sugu ziliandaliwa siku nyingi hivyo wanachofanya ni utekelezaji tu ambapo hadi sasa aneshavamia mikutano mitatu ya CCM ikiwa ni pamoja na kujipitisha pitisha wakati Mgombea Urais wa CCM Dk. Magufuli alipokuwa akihutubia katika viwanja vua Ruanda Nzovwe.
Alisema yote hayo majibu yake wanayo wakazi wa Jiji la Mbeya kwa kuamua kuchagua kati ya fujo au amani na kuingeza kuwa endapo atapewa ridhaa ya kuwa mbunge wa Mbeya mjini atahakikisha amani inapatikana ili machinga, Bodaboda, mama ntilie na wafanyabiashara waendeshe shughuli bila bugudha zozote.
Alisema atahakikisha viwanda vinafufuliwa ili vijana wengi wasio na kazi waweze kupata ajira ikiwa ni pamoja na kupunguza uhalifu kwa vijana wanaokosa kazi na kuzurura mitaani pia kuboresha miundombinu ya barabara zikiwemo kilomita kumi alizoahidiwa na mgombea Urais endapo atapita.
No comments:
Post a Comment