Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyirembe Munasa akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Benki ya Stanbic tawi la Mbeya katika hafla iliyofanyika hivi karibuni.
|
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyirembe Munasa akifungua kitambaa kuashiria ufunguzi wa jengo la Benki ya Stanbic tawi la Mbeya katika hafla iliyofanyika hivi karibuni.
|
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Nyerembe Munasa akitembezwa katika ofisi za benki ya Stanbic baada ya kuzindua rasmi kutokana na kukamilika kwa ukarabati.
|
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatiliakwa makini matukio yanayoendelea katika hafla ya uzinduzi watawi laMbeya.
|
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyerembe Munasa akimkabidhi zawadi mmoja wawateja wa Stanbic wakati wa hafla ya uzinduzi wa tawi laMbeya.
|
Mtendaji mkuu wa benki ya Stanbic akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi na viongozi wa Serikali baada ya sherehe za uzinduzi.
|
Mwenyekiti wa bodi ya benki ya Stanbic akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.
|
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi akiwaeleza waandishi wa habari kuhusiana na haliya usalama kwa wawekezaji ndani ya Mkoa wa Mbeya.
|
Meneja wa Benki ya Stanbic tawi la Mbeya Dismas Mathias akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyerembe Munasa |
Muonekano wa jengo baada ya ukarabati wa benki ya Stanbic jijini Mbeya.
|
Kikundi cha Makirikiri cha jijini Mbeya kikitoa burudani |
MKUU wa Wilaya ya Mbeya, Nyerembe Munasa amezitaka Benki zilizopo mkoani Mbeya kujikita katika kutoa elimu kwa wateja wao ili waweze kuwa wawekezaji katika miradi mbali mbali itakayoweza kukuza mitaji yao.
Nyerembe alitoa wito huo hivi karibuni alipomwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro katika hafla ya uzinduzi wa tawi la Benki ya Stanbic jijini Mbeya baada ya kufanyiwa ukarabati.
Alisema wananchi wasifundishwe kupewa mikopo bali elimu ya ujasiliamali na namna ya kuzalisha bidhaa kibunifu na kuwaandaa kuwa wawekezaji wa miradi ambayo wataifungua kwa msaada wa Benki.
“Tusiishie kuwapa samaki bali tuwafundishe namna ya kuvua kwa kuwapa ndoano hilo litasaidia kwa wao kuongeza uzalishaji kupitia kuwezeshwa kifedha kama ilivyo benki ya Stanbic” alisema Mkuu wa Wilaya.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi alisema kwa sasa wawekezaji mbali mbali wanakaribishwa mkoani Mbeya kuttokana na kuwa mji wenye amani ambao matokeo ya uhalifu yameisha kabisa tofauti na awali.
Aliongeza kuwa wakazi wa Mbeya hivi sasa wameelewa umuhimu wa uwekezaji ndiyo maana wameacha vitendo vya vurugu za mara kwa mara kwa kugundua kuwa kupitia wawekezaji wengi hupata ajira.
Aidha aliupongeza uongozi wa Stanbic kwa ukarabati wa jengo hilo ambapo alisema umesaidia kurahisisha shughuli za kiusalama na kulipunguzia kazi jeshi la Polisi kutokana na uimara wa jengo lilivyo.
Awali Mtendaji mkuu wa Benki ya Stanbic, Ken Cockerill alisema benki hiyo imedhamiria kutoa huduma bora kwa njia ya kisasa kwa wateja wake ikiwemo huduma nyinginezo za kibenki inayotokana na uzoefu wa kuhudumia wateja wake.
Alisema ubora wa benki hiyo hauko kwenye uzuri wa jengo bali hata kwenye huduma bora ili ziende samba mba na mahitaji ya wateja ili kuwarahisishia maisha na kuongeza kuwa hivi sasa benki tangu ifungue tawi lake mkoani Mbeya mwaka 2000 imefikisha wateja zaidi ya 5000.
Alisema mbali na ukarabati wa jengo pia imebadilisha mashine za kutolea fedha zilizokuwa kwenye vituo vyake na kufunga aina mpya zenye kioo cha kupangusa(touch screen).
No comments:
Post a Comment