Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, August 4, 2015

SHIRIKA LA HIFADHI ZA TAIFA(TANAPA) LAANZISHA KAMPENI YA UTALII WANDANI KWA WAZAWA.

 Kaimu Meneja masoko wa TANAPA, Victor Kitansi akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu kampeni ya kuhamasisha utalii wa ndani nchini.
 Maafisa Uhifadhi kutoka Hifadhi za Kitulo, Ruaha na Katavi wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na kampeni ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa Watanzania.
 Afisa TANAPA, Kanda ya Nyanda za juu kusini, Risala Kibongo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.
Baadhi ya Waandishi wa habari mkoani Mbeya wakiwa katika mkutano na maafisa wa Tanapa.

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa nchini(TANAPA) limeanzisha kampeni maalum ya kuwashawishi watanzania kutembelea hifadhi za Taifa ili kuongeza na kuhamasisha utalii wa ndani.
 
Akizungumza na waandishi wa habari wa Mkoa wa Mbeya, Kaimu Meneja Masoko wa TANAPA Makao makuu, Victor Katansi alisema kampeni hiyo itadumu kwa miezi sita ambayo ilizinduliwa Juni mwaka huu jijini Mwanza na Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu.
 
Alisema lengo la kampeni hiyo ni kuongeza idadi ya wananchi wanaotembelea hifadhi za taifa kutoka Watalii wa ndani 427408 wakiwemo wafanyakazi hadi kufikia 500,000 bila kujumuisha watumishi ifikapo Disemba mwaka huu.
 
Alisema kutakuwa nazawadi kwa mtanzania atakayetembelea Hifadhi kuanzia sasa ambapo atakayetembelea zaidi ya mara nne atajipatia zawadi ya juu kabisa ambapo atapelekwa kutalii katika hifadhi ya taifa ya Serengeti au Gombe na kulala katika hotel yenye hadhi ya nyota tano kwa siku tatu kwa gharama za Tanapa.
 
Alisema kwa atakayetembelea hifadhi zaidi ya mara tatu atajipatia CD za Wanyama, Tai na Tshirt la TANAPA, huku atakayetembelea zaidi ya mara mbili atajipatia CD za wanyama pamoja na Tshirt la TANAPA.
 
Kwa upande wake Afisa Mhifadhi wa TANAPA Kanda ya Nyanda za Juu kusini, Risala Kabongo alisema  mtanzania anaruhusiwa kutembelea sehemu yoyote ya hifadhi anayoona ipo karibu nae pia atapewa zawadi jizo.
 
Aliongeza kuwa pia kutatolewa zawadi kwa Taasisi au Kampuni au mtu binafsi atakayewapeleka watalii wasiopungua 1500 katika Hifadhi za Saa nane katika kipindi hiki cha kampeni na wasiopungua 150 kwa Mlima Kilimanjaro.
 
NA MBEYA YETU

No comments: