Mkuu wa banda la maonesho la nane nane la TTCL, Amos Gumbo(wa kwanza kushoto)akiwa pamoja na watumishi wa TTCL Mkoa wa Mbeya wakitoa ufafanuzi kwa wateja wao(hawapo pichani) kuhusiana na huduma mpya ya Televisheni.
Afisa wa TTCL ambaye jina lake halikupatikana mara moja akijaribu kuunganisha mitambo katika banda hilo ili kupata chaneli za televisheni bila kutumia king'amuzi.
Baadhi ya Chaneli za Televisheni zilizopatikana katika zoezi la majaribio ya kutumia internet kupata tv.
Baadhi ya mitambo itakayowawezesha wananchi kupata TV kwa njia ya Internet wakiwa majumbani.
KAMPUNI ya simu ya TTCL Mkoa wa
Mbeya inawakaribisha wakazi wa mikoa ya Nyanda za juu kutembelea banda la TTCL
katika maonesho ya nanenane yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale jijini
Mbeya kujionea huduma mpya.
Akizungumza na wananchi waliojitokeza
kuangalia huduma katika banda hilo, mkuu wa banda la maonesho la TTCL, Amos
Gumbo ambaye pia ni Kaimu Meneja msaidizi wa Biashara Mkoa wa Mbeya alisema
huduma mpya walioleta ni IPTV.
Gumbo alisema huduma hiyo
humuwezesha kila mtanzania kuangalia Televisheni kwa njia ya digitali
pasipokuwa na king’amuzi, Ungo wala antenna.
Alisema Internet Protocal
Television (IPTV) ni rahisi sana pia hulinda usalama wa mwananchi kwani
hatakuwa na vitu vya kumshawishi mwizi kumnyemelea kwani atatakiwa kuwa na vitu
vichache ili aweze kuangalia Chaneli mbali mbali za Tv.
Alivitaja vitu hivyo kuwa ni
pamoja na Televisheni ya kawaida, Laini ya simu ya Kampuni ya TTCL,Kompyuta ya
aina yoyote na kifurushi hivyo atakuwa na uwezo wa kuunganishiwa huduma hiyo.
Aliongeza kuwa huduma hiyo ni
nafuu sana na haina vitu vingi vinavyopaswa kuunganishiwa, ambapo mteja
atauziwa kwa gharama ndogo ukilinganisha na huduma zingine hivyo wananchi wote
mnaombwa kutembelea banda la TTCL kupata maelezo zaidi.
NA MBEYA YETU
No comments:
Post a Comment