Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa amesimama imara kupokea salam maalumu kutoka kwa askari wa magereza wakati wa mahafali ya kuhitimu mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi ya 21.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitoa heshima wakati wa mahafali ya kuhitimu mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi ya 21.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikagua gwaride la askari wa magereza wakati wa mahafali ya kuhitimu mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi ya 21.
Kiongozi wa Gwaride akitoa maelekezo kwa askari.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimtunuku cheo cha Ukoplo mmoja wa wahitimu kwa niaba ya wenzie wakati wa mahafali ya kuhitimu mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi ya 21.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitoa Cheti kwa mwanafunzi aliyefanya vizuri wakati wa mahafali ya kuhitimu mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi ya 21.
Kikosi cha Bendera kikipita mbele ya mgeni rasmi.
Gwaride likipita mbele ya mgeni rasmi kwa mwendo wa pole na kasi.
Waziri Mkuu akipita kukagua gwaride maalum.
Wahitimu wa mafunzo ya uongozi wakionesha umahiri wao wa ukakamavu kwa kuvunja vitu vigumu.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa meza kuu.
Brass band ya Magereza ikitumbuiza.
Wahitimu wakiwa kwenye gwaride maalum.
Watoto wadogo wakiwaimbia wahitimu wimbo wa kuwaaga.
Mkuu wa Chuo cha Magereza Kiwira, Tranford Mtilindula akisoma risala ya Chuo kwa mgeni rasmi.
Wahitimu wakiimba wimbo maalum katik mahafali yao.
Kamishna wa Magereza John Minja akimkaribisha mgeni rasmi kutoa hotuba na kufunga rasmi mafunzo.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Mbarak Abdulwakil akitoa salamu za Serikali.
Wahitimu wakiwa katika ukumbi wa mikutano.
Waziri mkuu akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya ulinzi na usala Mkoa wa Mbeya.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kushuhudia mahafali ya wahitimu wa mafunzo ya uongozi daraja la kwanza.
WAZIRI Mkuu Mizerngo Pinda amefunga
mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kwa Maaskari Magereza kozi namba 21 Kiwira
Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.
Akifunga mafunzo hayo pamoja na
kuwatunuku vyeo vya Ukoplo wa Magereza Waziri Mkuu aliwataka Maaskari Magereza
kuzingatia nidhamu katika kazi kuwa na uadilifu pamoja na kuzingatia haki za
binadamu na utawala bora wakiwa kazini.
Alisema Askari yeyote anapaswa
awe na nidhamu ya hali ya juu katika utekelezaji wa majukumu yake kwa kufanya
kazi kwa uadilifu na kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni jambo
litakalotoa mfano kwa askari wa ngazi za chini.
Alisema Tanzania imeridhia na
kusaini mikataba mbali mbali ya kimataifa kama mwanachama wa Umoja wa Mataifa
hivyo inapaswa kutekeleza kanuni hizo kwa kuhakikisha wafungwa wanahudumiwa kwa
kuzingatia misingi ya haki za binadamu.
Waziri Mkuu Pinda alilipongeza
Jeshi la Magereza nchini na kwamba ni mfano wa kuigwa katika baadhi ya Nchi
kutokana na kufanikiwa katika kipengele chja kuwarekebisha wafungwa na hatimaye
kuwa watu wema na kuacha uhalifu.
Alisema jukumu kubwa la Jeshi
la Magereza ni kurekebisha tabia za Wafungwawalioko magerezani jambo ambalo
hutekelezwa kwa kuwapatia ujuzi na stadi mbali mbali za kuwawezesha kupata
ajira halali wamalizapo vifungo vyao
sambamba na kuwapa ushauri nasaha wa kijamii, kisaikolojia na kiroho kulingana
na aina ya makosa.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo
cha Magereza Kiwira, Tranford Ntilindula, alisema mafunzo ya uongozi daraja la
kwanza kozi ya 21 yalianza juni 1, mwaka huu yakiwahusisha wanafunzi 713 lakini
waliuofanikiwa kuhitimu ni 711.
Alisema kati yao ni wanaume 625
na wanawake 86 ambao walipatiwa mafunzo katika Nyanja za utawala na uendeshaji
wa magereza,uongozi na utawala bora, sheria zinazoongoza Jeshi la Magereza,
ustawi wa jamii, uraia, afya na mafunzo ya kijeshi pamoja na madhara yatokanayo
na Rushwa.
Alisema Wanafunzi hao
walionesha nidhamu ya hali ya juu na kuzingatia masomo katika muda wote hivyo
kustahili kupandishwa vyeo na kuwa Koplo wa Magereza.
Aliongeza kuwa wanafunzi hao
walipokuwa masomoni walioonesha moyo wa kujitolea kwa kuchanga fedha taslimu
shilingi milioni 1,424,000 kwa ajili ya kununua umeme wa jua(solar power) kwa
matumizi ya Zahanati ya Chuo kwa ajili ya kukabiliana na tatizo la kukatika kwa
umeme wa Tanesco mara kwa mara.
Naye Kamishna wa Magereza
nchini, John Minja alisema Jeshi la Magereza likiwezeshwa linaweza hivyo
kuiomba serikali kuipa kipaumbele katika kufanikisha miradi mbali mbali
wanayoomba.
Kamishna Minja alimalizia kwa
kumuaga Waziri Mkuu Pinda katika utumishi wake Kwa Jeshi la Magereza kumpa
zawadi ya Mitamba miwili yenye mimba pamoja na mzinga wa nyuki kwa ajili ya
kuendeleza ufugaji pindi akistaafu.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment