Hii ndio hali halisi ya Barabara hii
WAKAZI wa Mtaa wa Tanesco Sae jijini Mbeya wameilalamikia barabara inayounganisha barabara ya Mwakibete ilipoishia lami na barabara kuu kituo cha Sae kuwa ni kibovu na kinawaletea usumbufu.
Wakazi wa mtaa huo walisema usumbufu wanaoupata kwa sasa ni kipande hicho cha barabara ambacho urefu wake hauzidi kilomita moja kujaa mashimo na vumbi jambo linalohatarisha kukatika kwa mawasiliano kipindi cha mvua.
Wakazi hao ambao hawakutaka kutaja majina yao walisema endapo kipande hicho kitaachwa hadi Novemba mwaka huu hakuna mtu atakayeweza kupita kwani hivi sasa hata watembea kwa miguu wanashindwa kupita kutokana na mashimo makubwa yaliyojaa vumbi.
Waliongeza kuwa usumbufu mwingine wanaoupata ni kutokana na vumbi kubwa kujaa majumbani mwao licha ya kufanya usafi kila mara hali inayoleta usumbufu na kushindwa kufanya shughuli zingine.
Hata hivyo juhudi za kuwapata viongozi wa Jiji kuzungumzia suala hilo hazikuzaa matunda kutokana na kukosekana kwa mawasiliano na kutokuwepo ofisini.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment