Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, August 13, 2015

HOT NEWS: WAFANYABIASHARA SIDO WAITUNISHIA MISULI HALMASHAURI JIJI LA MBEYA.

Hili Ndilo Soko Jipya la Mwanjelwa Soko la Kisasa ambalo ndilo linaleta Mushikeli na wafanyabiashara, Ikumbukwe hapa ndipo ambapo paliungua.

 Hapa Maduka yote upande wa Sido yamefungwa, Pako Kimya kabisa huku wafanyabiashara wote wakiwa katika mkutano na Halmashauri ya Jiji katika Ukumbi wa Mkapa.
 Mganga Mkuu wa Jiji Dkt. Samweli Lazaro akifafanua Jambo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Jiji
Mkurugenzi wa Jiji Mussa Zungiza akiwaeleza wafanyabiashara makubaliano mbalimbali yaliyofikiwa
 Mwenyekiti wa wafanya Biashara wa Mkoa wa Mbeya Charles Sionga akisisitiza jambo
 Katibu wa wafanyabiashara Mkoa wa Mbeya Allanus Ngogo akiuliza swali kwa niaba ya wafanyabiashara 
 Mmoja wa wafanyabiashara na Muhanga wa kuunguliwa na Soko la Mwanjelwa akiuliza swali
 Wafanyabiashara wa Soko la Mwanjelwa wakiwa katika mkutano na Jiji

Picha na Mbeya yetu

WAHANGA wa Soko la Mwanjelwa jijini Mbeya ambao wanafanyabiashara zao katika Soko la Sido wameitaka Halmashauri ya Jiji la Mbeya kutolifungua soko jipya hadi watakapopata eneo mbadala.
Wafanyabiashara hao wametoa kauli hiyo kufuatia Halmashauri kuwataka kujisajili kwa ajili ya kuingia kwenye soko jipya baada ya ukarabati wake kukamilika.
Aidha wafanyabiashara hao ambao ni wahanga wametakiwa kujaza fomu hizo hadi kufikia Agosti 17 mwaka huu ili waanze kufanya biashara zao mara moja kutokana na Halmashauri kuanza kulipa deni Agosti 30 mwaka huu.
Akizungumza katika mkutano na Wahanga hao katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Mkapa, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Musa Zungiza alisema wamelazimika kuanza kuwaruhusu mapema kutokana na kudaiwa mkopo uliotakiwa na Benki ya CRDB.
Zungiza alisema Benki inaitaka Halmashauri kupitia soko hilo kulipa deni la Shilingi Bilioni 25 kwa muda wa miaka 15 deni linalotakiwa kuanza mapema mwaka huu ili kuendana na kipindi hicho.
Alisema kutokana na ukubwa wa deni hilo Halmashauri pamoja na uongozi wa Wafanyabiashara ambao walipewa eneo la muda la Sido wamekubaliana kuwepo kwa utaratibu juu ya upatikanaji wa fedha za kulipa deni hilo.
Alisema utaratibu huo ni pamoja na kila mfanyabiashara atakayepewa chumba kwa ajili ya duka atalazimika kulipia shilingi Laki tano kwa mwezi huku mwenye kizima akilazimika kulipia ushuru wa shilingi 1000 kwa siku na wengine 15000 kutegemeana na biashara.
Aliongeza kuwa ili deni hilo liweze kupatikana na kukusanywa kwa wakati Halmashauri imeikabidhi jukumu hilo shirika la UTT ambalo litakuwa na jukumu la kukusanya ushuru, kusimamia usafi, umeme na huduma za maji ndani ya soko.
Alisema kwa utaratibu huo Halmashauri itatakiwa kuilipa  benki ya CRDB Shilingi Milioni 341 kila mwezi kwa muda wa miaka 15 ili kukamilisha deni lote hivyo kupitia wafanya biashara ambao ni wahanga ndiyo watakaolipa kupitia ushuru.
Akifafanua zaidi baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wafanyabiashara, Kwa niaba ya Mkurugenzi, Dk. Samwel Lazaro alisema uaratibu wa soko hilo utawapa kipaumbele wahanga ambao watatimiza masharti ya kulipa kiingilio ndipo watakapokaribishwa wengine.
Alisema wahanga ambao watakosa fedha hizo watatafutiwa eneo mbadala ambalo watakubaliana nalo kwa pamoja ili wahamie wote ikiwa ni pamoja na kuendelea katika eneo la sido ambalo walitakiwa kuwepo kwa muda.
Kwa upande wao wafanyabiashara hao wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Charles Syonga na Katibu Alanus Ngogo waliowataka viongozi wa Halmashauri kutokulifungua soko jiopya hadi pale eneo mbadala litakuwa limepatikana.
Walisema pia wafanyabiashara wakipatiwa eneo waachiwe walijenge wenyewe pampoja na kuandikishana mikataba ya kisheria ili kuepuka kuhamishwa hamishwa mara kwa mara.
Akijibu maswali hayo kwa niaba ya Mkurugenzi, Dk. Lazaro alisema eneo la Sido linamgogoro ambao kesi yake iko mahakamani lakini wahanga hao hawataondoka eneo hilo hadi hapo sehemu mbadala itakuwa imepatika.
Alisema kuhusu eneo mbadala itategemea ni wahanga wangapi waliokosa sifa kwa Halmashauri inawatambua waliounguliwa tu ambao ni 960 na sio zaidi ya hapo ambapo pia alitoa wito kwa wafanyabiashara wengine kutumia mgongo wa wahanga kujipaia maeneo.
Aliongeza kuwa kuna baadhi yaw au wanatumia jina la Mkurugenzi kutapeli wafanyabiashara kwa kuwalipisha fedha ili wapatiwe maduka jambo aliloswema ni utapeli na tayari ameshakamatwa mmoja na kufikishwa polisi.


No comments: