Naibu waziri wa
Viwanda na Biashara, Janet Mmbene, (wapili kushoto), akipeana mikono na Meneja
msaidizi wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, tawi la Tunduma, Teddy Msanzi, wakati
wa hafla ya kukabidhi madawati yaliyotolewa kama msaada na benki hiyo, kusaidia
shule mbili za msingi wilayani Ileje, mkoa wa Mbeya, hivi karibuni
NA K-VIS MEDIA
Benki
ya Posta Tanzania (TPB) kupitia tawi lake la Tunduma, imetoa msaada wa madawati
100 yenye thamani ya shilingi Milioni Tatu kwa shule mbili za Msingi zilizopo
Wilayani Ileje, mkoani Mbeya.
Akikabidhi
madawati hayo kwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Janeth Mbene kwenye
hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika Wilayani humo hivi karibuni, Meneja wa
Benki ya Posta Tawi la Tunduma Teddy Msanzi alisema kuwa, Benki yake iliguswa sana na suala la uhaba wa
madawati kwa wanafunzi wa Wilaya hiyo na kuona ni muhimu kusaidia.
“Benki
ya Posta inatambua umuhimu wa elimu bora kwa ajili ya kujenga kizazi bora cha
baadae. Ni vigumu kutoa elimu bora katika mazingira magumu ya wanafunzi kukaa
chini madarasani.Ni vema wanafunzi wetu wakawekewa mazingira mazuri ya kupata
elimu, ikiwemo madawati. Hivyo basi sisi Benki ya Posta tunatoa madawati haya
100 ili kupunguza tatizo hili.” Alifafanua Teddy.
Kwa
mujibu wa taarifa ya ofisi ya elimu wilaya Ileje, Wilaya hiyo ina jumla ya
wanafunzi 28,488 wa shule za Msingi , lakini idadi ya madawatii ni 10,028, na
kufanya idadi ya madawati yanayohitajika kuwa 4,116.
Akitoa
shukrani zake kwa niaba ya shule za Wilaya ya Ileje, Mhe. Janeth Mbene aliishukuru
Benki ya Posta kwa msaada huo ambao alisema ni mkombozi kwa wanafunzi waliokuwa
wakikaa chini kwa muda mrefu. Alitumia fursa hiyo pia kuziomba taasisi nyingine
ziguswe na tatizo lao na ziweze kuwasaidia ili waweze kuondokana na changamoto
hiyo.
Naibu Waziri Mmbene, akiwa na maafisa wa benki hiyo, tawi la Tunduma
Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene akimkabidhi katibu wa CCM Wilaya ya
Ileje Hamida Mbogo madawati ya kwa ajili ya shule za sekondari na msingi
wilayani ileje ambayo yametolewa na benki Posta Tawi la Tunduma.
No comments:
Post a Comment