Add caption |
SEHEMU ya wana-CCM wa kata ya Nsalaga
|
MWENYEKITI wa UVCCM mkoa wa Mbeya, Aman Kajuna, naye akipiga magoti kuomba kura |
MWENYEKITI wa Jumuia ya Wazazi ya CCM mkoa wa Mbeya, Fatuma Kasenga
akiomba kura
|
Makada hao walilazimika kupiga magoti, kugalagala ardhini, kulazimisha kuulizwa
maswali, ili mradi wapiga kura wawaonee huruma na kuwachagua.
Hayo yalijiri wakati makada hao, wanaowania kuomba kuteuliwa na CCM wilaya ya Mbeya mjini, walipokuwa wakijinadi kwa wana-CCM wa kata ya Nsalagha,ili kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuipeperusha bendera ya CCM.
Fatuma ambaye hii ni mara yake ya pili kujitokeza kuwania ateuliwe na CCM
kuwania ubunge jimbo la Mbeya mjini, alisema mwaka 2010 kura zake hazikuweza
kutosha hivyo kuwaomba wana-CCM wasimuangushe mwaka huu.
Aliongeza lengo la kujitokeza kuwania nafasi hiyo ni kutaka kurudisha heshima ya jimbo la Mbeya, ambayo hivi sasa imepotea baada ya jimbo hilo kuwa chini ya mbunge wa kutoka chama cha upinzani kwa miaka mitano sasa.
Fatuma ambaye alikuwa akijinadi huku akiwa amepiga magoti, ambapo mara baada ya
kumaliza dakika zake tatu alizokuwa amepewa pamoja na kujibu maswali
aliyoulizwa, ndipo alipoanza kugalagala huku akiomba kura kwa wana-CCM.
Hatua hiyo iliwafanya baadhi ya viongozi waliokuwa meza kuu, kulazimika
kusimama na kwenda kumsaidia kumuinua kasha kumsindikiza walipokuwa wamepangiwa
kukaa wagombea wenzake.
Naye Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Mbeya, Aman Kajuna, alisema wakati
anachaguliwa kushika nafasi hiyo mwaka 2012, alikuta asilimia kubwa ya vijana
ndani ya jiji la Mbeya wakiwa wamekata tamaa na kuhamia upinzani.
Kajuna alisema kazi yake ya kwanza ilikuwa ni kuwafikia vijana hao akianzia na
wale wa CCM, kukaa nao na kuwauliza sababu iliyopelekea wakate tamaa na Chama,
ambapo aliwaomba warudi kukitumikia na kukitetea Chama.
Mara baada ya kumaliza kujinadi kwa wana-CCM hao, Kajuna aliamua kupiga magoti na kuomba kura akiwaahidi wanachama hao kuwa anao uhakika wa asilimia nyingi kuwa anao uwezo wa kulikomboa jimbo hili, kwani ametoa misaada mingi kwa vijana, wanawake na wazee.
Kwa pande wake Mkurugenzi wa kituo cha radio Generation Fm, kilichopo jijini
Mbeya, Shadrack Makombe, alisema yeye ni kijana wa viwango, hivyo kuwaomba
wana-CCM wamchague ili kuipeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi mkuu wa
mwaka huu.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment