Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, July 24, 2015

ASKARI MGAMBO WAZIFUNGA OFISI ZA HALMASHAURI YA MBEYA WAKISHINIKIZA KULIPWA.


Mgambo wa Almashauri ya jiji la Mbeya wakiwa wameweka ulinzi mkali katika geti kuu la kuingilia wafanyakazi..(Picha na David Nyembe wa Fahari News)

Wafanyakazi wa Almashauri ya jiji la Mbeya wakiwa wamesimama nje wakisubiri nini kitaendelea..(Picha na David Nyembe wa Fahari News)

Mgambo wa almashauri wakielekea kufungua Mageti mara baada ya kukubaliana na Mkurugenzi wa Jiji.(Picha na David Nyembe wa Fahari News)
Wafanyakazi wakikimbia camera mara baaada ya kufunguliwa Geti.(Picha na David Nyembe wa Fahari News)ASKARI mgambo wa halmashauri ya Jiji la Mbeya,leo wamefunga geti kuu la ofisi za halmashauri ya Jiji na kuzuia wafanyakazi kushindwa kuingia ndani wakishinikiza kulipwa mishahara yao ya miezi miwili pamoja na kutatuliwa kwa kero mbalimbali zinazowakabili askari hao.
Askari hao zaidi ya 20 wakiwa ndani ya ofisi za halmashauri hiyo, waligoma kufungua geti kuu hilo kwa zaidi ya masaa mawili na kusababisha kero kwa watumishi na wateja mbalimbali ambao waifika kupata huduma.
Akizungumza na Mtanzania,mmoja wa kiongozi wa askari hao Athanas Samsoni, alisema wao wameamua kufunga geti hilo na kuzuia watumishi kwa lengo la kuushinikiza uongozi ambao ndio mwajiri wao kuwalipa mishahara yao pamoja na posho mbalimbali.
Alisema, mbali na madai hayo pia mwajiri huyo amekuwa akishindwa kuwashonea sare za kazi jambo linalosababisha kujitegemea hivyo kuendelea kuwaweka kwenye mazingira magumu ya kiuchumi.
Alisema, wao wanachokihitaji kutoka kwa mwajiri wao ni kulipwa mishahara yao pamoja na kutekelezewa mahitaji yao muhimu kama vile sare na posho.
Akizungumzia tatizo hilo, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Dk. Samweli Razalo alikiri kwa halmashauri hiyo kutowalipa mishahara askari ho mgambo na kwamba suala lao linashughulikiwa.
“Madai yao ni ya msingi na wanaidai halmashauri mshahara wa miezi miwili Mei na Juni, uongozi ulishakaa na viongozi wa askari na kuwaeleza lakini tunashangaa kuona leo wamechukua uamuzi wa kufunga geti,”alisema.
Mwisho.

No comments: