Nwaka
Mwakisu akiwa kwenye ofisi za Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mbeya mjini tayari
kuchukua fomu.
|
Nwaka
Mwakisu akimkabidhi fedha Katibu Msaidizi wa CCM Wilaya ya Mbeya kwa ajili ya
fomu za kuwania kuteuliwa kugombea ubunge.
|
.Mwakisu
akisaini daftari maalum baada ya fedha zake kupokelewa.
|
Mwakisu
akikabidhiwa fomu baada ya kukamilisha taratibu zote.
|
Mwakisu
pamoja na mkewe wakitoka kwenye ofisi za Chama baada ya kuchukua fomu.
|
Nwaka
Mwakisu akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu nia yake ya kutaka kuteuliwa
kugombea Ubunge.
|
Baadhi
ya waandishi wa habari pamoja na wananchi wakimsikiliza Mwakisu akieleza
malengo yake.
|
MJUMBE
wa Mkutano Mkuu(CCM)kupitia Umoja wa Vijana Mkoa wa Mbeya, Nwaka Mwakisu
amejitosa na kuchukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea Ubunge katika Jimbo la
Mbeya Mjini(CCM).
Akizungumza
na waandishi wa habari baada ya kuchukua Fomu hizo, Mwakisu alisema endapo
Chama kitampitisha na hatimaye kushinda Ubunge hata kuwa na muda wa kutoa ahadi
kwa wananchi wa Jiji la Mbeya bali vitu vingi ameshavifanya kilichobakia ni
utekelezaji tu.
Alisema
idadi kubwa ya wagombea waliojitokeza asilimia kubwa hawaijui Mbeya pamoja na
wakazi wake wanachokihitaji jambo lililopelekea kuwepo kwa vurugu za mara kwa
mara kutokana na vijana kutokuwa na Mwakilishi anaewafahamu.
Alisema
yeye anajivunia rekodi na mazuri aliyowafanyia vijana na wananchi kwa ujumla wa
Jiji la Mbeya yakiwemo ya kuwaunganisha vijana waendesha bodaboda na bajaji
ambao tayari wanavyama vilivyosajiliwa na kutambuliwa kisheria.
Alisema
kwa upande wa Wanawake na wananchi wengine wakiwomo wafanyabiashara ndogondogo,
machinga na watumishi wa umma na mashirika binafsi tayari ameanzisha Benki
itakayojulikana kwa jina la Mbeya Youth Microfinance Bank ambayo iko katika
hatua za mwisho.
Aliongeza
kuwa Benki hiyo itakuwa ya manufaa kwa wananchi wote wa Jiji na Mkoa wa Mbeya
ambapo wataweza kupata mikopo nafuu ya fedha pamoja na vitendea kazi huku
akitanabaisha kuwa endapo atapata nafasi ya kuwa Mbunge mishahara yake yote
itapitia kwenye akaunti ya Benki hiyo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment