Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, July 7, 2015

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MRADI MKUBWA WA UFUGAJI SAMAKI RUNGWE.


Mkurugenzi mtendaji wa Riverbanks fish farm,Kenny Nyambacha, akisoma taarifa mbele ya Mwenge wa Uhuru ulipofika kuzindua mradi mkubwa wa ufugaji samaki Ilundo Kiwira wilayani Rungwe.


Mkurugenzi mtendaji wa Riverbanks fish farm,Kenny Nyambacha, akimkabidhi taarifa kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, Juma Khatibu Chum.


   Mkurugenzi mtendaji wa Riverbanks fish farm,Kenny Nyambacha akipongezana na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Mwalimu Zainabu Mbusi.


Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Juma Khatibu Chum akizindua Mradi mkubwa wa ufugaji samaki.


    Mkurugenzi mtendaji wa Riverbanks fish farm,Kenny Nyambacha, akifafanua jambo kwa Wakimbiza Mwenge kitaifa.



Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Mwalimu Zainabu Mbusi akitoa neno la pongezi kwa mjasiliamali wa Samaki.



Kiongozi wa Mbio za Mwenge akitoa salamu kwa wakazi wa kijiji cha Ilundo kata ya Kiwira waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa mradi wa ufugaji wa samaki.

Mkurugenzi mtendaji wa Riverbanks fish farm,Kenny Nyambacha akipokea Mwenge wa Uhuru.


Mkurugenzi mtendaji wa Riverbanks fish farm,Kenny Nyambacha akiwa ameushika Mwenge wa Uhuru.


  Meneja wa Mradi wa Samaki, Denis Nyambacha akiwa ameshika Mwenge.


Mkurugenzi mtendaji wa Riverbanks fish farm,Kenny Nyambacha akionesha samaki aina ya Kambare anaowafuga katika mabwawa yake.

.                     Sehemu ya mabwawa


.                     Ngoma ya Wanyakyusa ikitoa burudani katika sherehe hizo.
 

WATANZANIA wametakiwa kuiga jitihada zinazofanywa na wengine katika kujiingizia vipato ili kuondokana na wimbo la umaskini.



Aidha wametakiwa kutumia changamoto zinazikabili jamii kubuni miradi mbali mbali inayoweza kuwaingizia vipato na sio kubweteka na kusubiria ajira kutoka serikalini.



Wito huo ulitolewa  na mkimbiza Mwenge wa Uhuru, Karim Mzee alipokuwa akizungumza kwa niaba ya kiongozi wa Mbio za mwenge kitaifa, Juma Khatibu Chum wakati Mwenge ulipokuwa ukizindua mradi mkubwa wa ufugaji samaki wa Riverbanks fish farm uliopo katika kijiji cha Ilundo Kiwira wilayani Rungwe.



Kiongozi huyo alisema mradi wa samaki umetokana na changamoto kubwa ya wananchi kupenda kutumia samaki kama kitoweo jambo lililomsukuma mtu huyo kutengeneza na kutoa wito kwa wengine kuiga mfano huo na kuanzisha miradi mingine.



Alisema tangu Mwenge uwashwe na kuanza kukimbizwa Aprili 29 mwaka huu hawajakutana na mradi mwingine mkubwa wa ufugaji wa samaki badala yake wengi wamekuwa na miradi ya kuigana kama ufugaji wa kuku na mifugo mingine.



Naye Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Mwalimu Zainabu Mbusi alisema wanawake wanapaswa kuacha tabia ya kuwategemea wanaume wao kwa kila kitu bali wanapaswa kugawana majukumu kama ilivyooneshwa na mmiliki wa mabwawa ya samaki ambaye mumewe yuko mbali nay eye akiendesha mradi mkubwa eneo lingine.



Awali akitoa taarifa mbele ya Mwenge wa uhuru, Mkurugenzi mtendaji wa Riverbanks fish farm,Kenny Nyambacha, alisema mradi huo ulianza mwaka 2009 ambapo hadi sasa umegharimu zaidi ya shilingi Milioni 77 na matarajio ni kufikia milioni 100 hadi kukamilika.



Alisema mradi una mabwawa 12 yenye ukubwa wa mita za mraba 10,118 pamoja na miti iliyopandwa 3500 kwa ajili ya kuhifadhi unyevu katika maeneo ya mradi na mazingira yanayolizunguka.



Alisema hivi sasa kuna jumla ya samaki 30000 aina ya sato na Kambare ambao huvunwa kila baada ya miezi nane wakiwa na uzito wa gramu 300 hadi gramu 800 ambapo mauzo yake hufanyika kwa jumla nareja reja katika masoko ya ndani na nchi Jirani za Malawi na Kongo.



Aliongeza kuwa matarajio yake ni kufungua kituo cha mafunzo kwa ajili ya kuiwezesha jamii inayomzunguka ili kupata elimu juu ya ufugaji wa samakikewa njia ya mabwawa kutokana na eneo hilo kujaaliwa kuwa na maji mengi ili kupunguza adha ya kitoeo katika kaya.



Mwisho.
Na Mbeya yetu


No comments: