|
Plant Meneja wa Tbl Mbeya, Waziri Jemedari akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na siku ya Familia iliyofanyika Ifisi Mkoani Mbeya. |
|
Mkuu wa Matukio wa TBL Kanda ya Nyanda za juu kusini, Abubakar Masoli akielezea umuhimu wa wafanyakazi kukutana na familia zao na kufurahi pamoja. |
|
Baadhi ya Wafanyakazi wa TBL wakibadilishana mawazo katika sherehe za siku ya familia |
|
Wanafamilia wa TBL wakiwa wamejumuika na Watumishi wa TBL katika sherehe za siku ya familia |
|
Wafanyakazi wa TBL Mbeya wakiwa kwenye sherehe za familia |
|
Baadhi ya Wanafamilia wa TBL wakiendelea na michezo |
|
Wazazi na watoto wakiingia kwenye viwanja vya sherehe |
|
Baadhi ya wanafamilia wakiingia katika viwanja vya Ifisi pamoja na familia zao kwa ajili ya sherehe |
|
Watoto wakiendelea na michezo. |
WAFANYAKAZI wa kampuni ya Bia ya TBL Mbeya wameungana na familia zao katika sherehe za familia zilizofanyika katika viwanja vya ukumbi wa mikutano wa Ifisi(ICC) Mbalizi wilaya ya Mbeya.
Akizungumza katika sherehe hizo, Meneja wa Kiwanda cha Mbeya(Plant Meneja), Waziri Jemedari amesema lengo la kuweka sherehe ni kuhakikisha Wafanyakazi pamoja na familia zao wanakutana angalau mara moja kwa mwaka ili kufahamiana na kujenga undugu.
Amesema Wafanyakazi mara nyingi hukutana wakiwa kazini lakini watoto, wake na waume zao hawafahamiani hivyo kupitia siku ya familia husaidia kujenga uhusiano na kufanya kuwa familia moja.
Aidha ametoa wito kwa wazazi nchini kuacha tabia ya kuwatuma watoto waliochini ya umri wa miaka 18 kununua ama kushika pombe kwa kile alichodai wanajifunza tabia mbaya ambayo inawaathiri katika makuzi yao.
Amesema watoto wanapaswa kufundishwa na kuelezwa mapema uzuri, ubaya na madhara ya pombe wakiwa bado na umri mdogo kwa kuwazuia hata kugusa.
Ameongeza kuwa watumiaji wa Bia zinazozalishwa na Kiwanda cha Mbeya wajivunie kutumia bia zenye ubora na kiwango cha juu baada ya Bia yao aina ya Castle lager kupata matokeo ya 9.7 kati ya 10 kwa Afrika nzima.
Amesema katika kujiridhisha na ubora huo ni vema wateja wakajikusanya kwenye makundi na kutoa taarifa wa kiwanda ili waweze kutembelea na kujionea uzalishaji unavyofanyika kiwandani hapo.
No comments:
Post a Comment