Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Anderson Kabenga akihutubia mkutano wa hadhara.
Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbeya wakiwa wamekaa meza kuu.
Mjumbe wa Mkutano mkuu, Mchungaji Jackob Mwakasole akimkabidhi kadi ya chama mwanachama mpya, Benson Mwakilembe.
Mwanachama mpya, Benson Mwakilembe akipongezwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Mbeya.
Baadhi ya wanachama wa CCM wakiwa katika mkutano wa hadhara
VYAMA vya upinzani
vimetakiwa kujikita zaidi katika kukisoa Chama tawala ikiwa ni pamoja na
kueneza sera zinazoweza kuwakomboa wananchi kutoka hapa walipo na kusongambele
tofauti na ilivyosasa ambapo wamejikita kupotosha na kueneza chuki.
Wito huo ulitolewa na
mjumbe wa mkutano mkuu wa taifa wa CCM kupitia Wilaya ya Mbeya vijijini,
Mchungaji Jackob Mwakasole, alipokuwa akihutubia wananchi katika mkutano wa
hadhara uliofanyika katika viwanja vya mahubiri Mbalizi wilayani Mbeya.
Mwakasole alisema mikutano ya vyama vya upinzani imejaa
chuki ambazo wanazipandikiza kwa wananchi ili wakichukie Chama tawala bila
kuwaeleza ukweli wa mambo mazuri yaliyokwisha fanyika na kueleza sera zao.
Alisema lengo la mikutano ni
kuwaeleza wananchi juu ya mambo yaliyofanyika ya ukweli lakini wapinzani
wanasahau kazi yao ya kukikosoa Chama tawala na badala yake wamekuwa wakitumia
nguvu nyingi na mabavu kutaka kuingia madarakani.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Mbeya, Anderson Kabange alisema Halmashauri imepata hati safi
kwa miaka mitano mfululizo kutoka kwa mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za
serikali(CAG) na ndiyo maana miradi mipya inaletwa.
Alisema wapinzani wanasema
Serikali imechakachua ujenzi wa barabara za lami katika mji mdogo wa Mbalizi
lakini wameshindwa kutoa takwimu sahihi juu ya fedha zilizotolewa na kiwango
cha barabara kilichojengwa kutokana na kushindwa kufanya utafiti.
Alisema kudumu kwa barabara
kutategemea kama masharti yaliyowekwa yatazingatiwa ikiwa ni pamoja na
kutopitisha magari makubwa yaliyozidi uzito uliopendekezwa na kwamba
atakayebainika kupitisha gari zito atatozwa faini ya shilingi 300,000 na
kifungo jela.
Aidha katika mkutano huo wanachama
wapya wa Chama cha Mapinduzi walikabidhiwa kadi wakiongozwa na mfanyabiashara
maarufu katika mji wa Mbalizi, Benson Mwakilembe ambaye awali ilisemekana
alikuwa akikifadhili chama cha Demokrasia na maendeleo.
Akizungumza baada ya
kukabidhiwa kadi, Mwakilembe alisema kwa muda mrefu amekuwa akisaidia shughuli
za maendeleo katika mji mdogo wa Mbalizi lakini amekuwa akihusishwa na Chadema
jambo ambalo ameamua kuliepuka kwa kuchukua kadi rasmi ya CCM.
Alisema hatoacha kukisaidia
Chama cha mapinduzi katika harakati za kuwaletea maendeleo wananchi na yupo
tayari kutoa magari yake muda wowote itakapohitajika kwa ajili ya maendeleo ya
wananchi.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment