Mwenyekiti
wa Chama cha Msalaba mwekundu Mkoa wa Mbeya, Ulimboka Mwakilili
akifungua mafunzo kwa wanachama wa Redcross Mkoa wa Mbeya.
Mkurugenzi
wa maendeleo ya Mikoa na Matawi wa Tanzania Redcross Society, Julius
Kejo akitoa mada katika mafunzo ya wanachama wa msalaba mwekundu Mbeya.
Mratibu wa Redcross Zanzibar, Ubwa Suleiman akitoa mafunzo kwa wanachama wa msalaba mwekundu Mbeya.
Viongozi wa Redcross wakifuatilia jambo.
Mwezeshaji
Renatus Mkaluka akielezea jambo kwa washiriki wa mafunzo ya kujiandaa
ili kuweza kukabiliana na dharura zitakazojitokeza.
Washiriki wa mafunzo wakiwa darasani.
Washiriki wa mafunzo wakionesha namna ya kusalimiana kwa kutumia salamu ya Redcross.
CHAMA cha Msalaba mwekundu
nchini (Redcross) kimetoa mafunzo kwa wanachama wake Mkoani Mbeya ya kujiandaa ili kuweza
kukabiliana na dharula mbali mbali zinazojitokeza(EPR).
Akizungumza wakati wa ufunguzi
wa mafunzo, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mikoa
na Matawi wa Chama cha Msalaba mwekundu, Julius Kejo, alisema mafunzo hayo
yanayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Mbeya Paradise yatadumu kwa muda wa
siku nne yenye lengo la kuwakumbusha wananchama kuwa tayari wakati wowote.
Kejo alisema katika mafunzo
hayo yaliyojumuisha Wanachama 20 watajifunza Historia ya Msalaba mwekundu
duniani, Historia ya msalaba mwekundu Tanzania na shughuli zake, vipaumbele vya
msalaba mwekundu pamoja na vitendea kazi vyake.
Alisema Chama cha Msalaba
mwekundu Tanzania kilikuwepo tangu kabla ya uhuru lakini kilianzishwa rasmi kwa
mujibu wa sheria ya Bunge namba 71 ya
mwaka 1962 ambapo mwaka 1963 Tanzania ilijiunga na Shirikisho la Msalaba mwekundu
duniani pamoja na Kamati ya kimataifa.
Alisema dhamira ya Chama cha
Msalaba mwekundu nchini ni kuhamasisha upatikanaji wa rasilimali kwa kutumia
nguvu ya ubinadamu kwa ajili ya kuboresha maisha ya watu wenye madhila mbali
mbali.
Aliongeza kuwa dira ya Chama
hicho ni kuwa na chama imara chenye ubora na kinachotegemewa katika kusaidia
serikali kufikia malengo yake ya kijamii, kiuchumi na maendeleo katika kutoa
huduma bora za kibinadamu nchini.
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa
majukumu ya Chama cha Msalaba mwekundu nchini wakati wa vita ni kusaidia
wagonjwa, majeruhi na wafungwa wa kivita na raia wengine walioathiriwa na madhara
ya vita pia kushiriki katika shughuli za kuboresha afya ya jamii, kuzuia
magonjwa na kupunguza madhila yake.
Alisema shughuli zingine ni
pamoja na kushiriki katika kazi zingine muhimu na zenye manufaa kwa jamii kadri
hali inavyojitokeza na namna kadri hali inayoruhusu.
Kwa upande wake mwezeshaji wa
mafunzo hayo, Ubwa Suleiman ambaye pia ni Mratibu wa Redcross Zanzibar alisema
ni kosa la jinai kwa baadhi ya taasisi kutumia nembo za Chama cha Msalaba
mwekundu bila utaratibu.
Alisema nembo za Chama hicho
hutumika kutambulisha wakati wa amani na wakati hakuna vita pia hutumika kama
ulinzi na kinga ambapo mwenye alama hizo haruhusiwi kushambuliwa wakati wa
vita.
Alisema alama zinazotumika na
Chama hicho na ambazo hutambuliwa kimataifa ni pamoja na msalaba
mwekundu(Redcross), Hilali nyekundu (Red crescent), alama ya jua na samba mwekundu
pamoja na alama ya fuele nyekundu(Red crystal).
Na Mbeya Yetu
No comments:
Post a Comment