Wananchi wa Kijiji cha Idimi Kata ya Ihango, wilaya ya Mbeya, wakimbeba mgonjwa kwa kutumia Machela kwenda Zahanati ya kawatele yenye umbali wa kilometa 10 |
Diwani wa Kata ya Ihango Fosta
Mwalingo alipinga wananchi wake kubebwa kwenye machela lakini
alipobanwa zaidi na maswali ya waandishi wa habari alishindwa
kutetea hoja yake.
|
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Marselin Mlelwa akiongea na waandishi wa habari kijijini hapo |
Wananchi wa Kijiji cha Idimi
Kata ya Ihango, wilaya ya Mbeya, wanalazimika kutembea umbali mrefu
kufuata huduma za matibabu huku wagonjwa wao kuwabeba kwenye machela
kwenda katika zahanati ya Kawetele.
Mwandishi wa habari hizi alishudia
wananchi wakijiji hicho wakiwa wamembeba wenzao kwenye machela wakimpeleka
katika Zahanati ya Kawetele umbali wa zaidi ya kilomita 10.
Wakizungumza na Mbeya yetu,
kijijini hapo wananchi hao
walisema licha ya kijiji hicho kuwa makao makuu ya Kata lakini wamekuwa
wakisafiri umbali wa zaidi ya kilomita 10 kufuata huduma za matibabu kwa
miaka mingi jambo ambalo walidai wamewapoteza ndugu zao kwa nyakati tofauti.
Mkazi wa kijiji hicho, Rose Sumuni
alisema kina mama wajawazito wamekuwa wakiteseka hususani
wakati wa kujifungua ambapo wengine wamekuwa wakijifungulia njiani na
wengine kupoteza maisha wao wenyewe ama watoto wakiwa tumboni.
“Binafsi nilimpoteza mtoto wangu
akiwa tumboni, kutokana na umbali wa zahanati ama kituo cha afya kuwa mbali,
ambapo hadi kufika Hospitali ya rufaa ya Meta na kufanyiwa oparesheni nilikuta
mtoto wangu amekufa” alisema mama huyo.
Mkazi mwingine Mashaka
Saagaje, alisema kutokana na kutokuwa na huduma yoyote ya matibabu
kila kitongoji walitengeneza machela maalum kwa ajili ya kubebea
wagonjwa.
“kwa kweli tunashida kubwa sana, mama
zetu wanapoteza maisha kutokana na miundombinu ya barabara kuwa mbovu na
kutembea mwendo mrefu ambapo tukichoka huwa tunamtua popote ili kupumzika
halafu tunaanza tena safari hadi zahanati ya Kawetele” alisema Saagaje.
Mwenyekiti wa Kjiji hicho,
Langson Paul alikiri wananchi wake kubebwa kwenye machela na kusafiri
mwendo mrefu kufuata huduma ya matibabu huku akibainisha kwamba kuna jengo la zahanati
ambalo lilijengwa kwa nguvu za wananchi wenyewe mwaka 2013 na kufikia usawa wa
mtambaa wa panya lakini wanashindwa kuendelea kutokana na ukata wa fedha.
Wakati wananchi wakitoa malalamiko
yao na mwenyekiti wao kukiri hivyo, Diwani wa Kata hiyo Fosta
Mwalingo alipinga wananchi wake kubebwa kwenye machela lakini
alipobanwa zaidi na maswali ya waandishi wa habari alishindwa
kutetea hoja yake.
‘Aaa!!! Sio kweli kwamba bado
tunabeba wagonjwa kwenye machela kwani hivi sasa tuna usafiri wa bajaji na
pikipiki, lakini jitihada zinaendelea kufanyika kuhakikisha tunamaliza zahanati
ambayo imejengwa na wananchi wenyewe” alisema diwani huyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Mbeya, Marselin Mlelwa alisema katika halmashauri hiyo kuna
vijiji vingi ambavyo wananchi wamejenga zahanti hadi kufikia usawa wa renta
hivyo kazi yao kubwa ni kumalizia wapofikia wananchi hivyo wanazipa kipaumbele
zahanati ambazo zipo mbali zaidi na vituo vya afya ama zahanati jirani.
“Unajua hili ni agizo la Rais kwamba
wananchi wajenge hadi usawa fulani halafu serikali inamalizia, na tumeanza
kufanya hivyo, lakini hapa tunaangalia zaidi vijiji ambavyo vipo mbali zaidi na
hospitali ya rufaa, mkoa au vituo vya afya lakini kwa hapa Idimi sio mbali na
hospitali ya rufaa na mkoa” alisema Mlelwa.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment