MSTAHIKI Meya wa Jiji la Mbeya,
Athanas Kapunga, amesema hana sababu ya kuendelea kujibizana na
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (Chadema), kwani amekuwa
akimpa changamoto za kiutendaji ambazo zimemfanya kufanya kazi kwa ufanisi.
Amesema, mbunge huyo anaapswa
kusubiri kubali cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ili aweze kutumia vema
jukwaa la kisiasa kuliko ilivyo sasa anavyotumia Bunge kuwachafua watu wengine.
Akizungumza na waandishi wa habari
jana mjini Mbeya, Meya Kapunga, alitumia nafasi hiyo kutoa ufafanuzi
kuhusu hali halisi ya utendaji kazi wake uliokuwa umezungukwa na majungu, chuki
na fitina zisizokuwa na msingi zinazoendelea kutolewa na Mbunge ‘Sugu’
ambaye alimfananisha sawa na chipukizi wa kisiasa.
“Leo (jana), asubuhi
nimemsikia Sugu, akizungumza bungeni kuhusu ugawaji wa Jimbo la Mbeya Mjini na
kunitaja mimi ni miongoni mwa viongozi wanaoshinikiza kugawanywa kwa jimbo
hili, wala sikatai ni kweli kwani mchakato huu wa kuligawa jimbo hili niwa muda
mrefu kabla ya Sugu kuingia ulingoni,” alisema
Kapunga
Alisema, mchakato wa kuligawa jimbo
hilo, ulianza mwaka 2008 ukiwa chini ya Mbunge Mpesya hivyo yeye kama
Meya ni jukumu lake kulisemea hilo kama mtendaji wa halmashauri.
“Hapa kosa langu nini mpaka Sugu kunisema
bungeni, kwanza nimeona ni mtoto anayezoea tabia mbaya, kukaa kila saa
ananisema bungeni anaonyesha ni jinsi gani asivyokomaa kisiasa,” alisema
Alisema, Sugu ni mjumbe wa vikao vya
kiutendaji vya halmashauri ana nafasi kubwa ya kufika na kuyazungumzia hayo
tatizo linalomsumbua ni upeo wake mdogo wa kufikiri hivyo kujiaminisha
kwambajimbo la Mbeya ni mali yake.
Alisema, Mbeya ni mali
ya wananchi, si la ukoo na kitendo cha kuwaza jimbo ni mali yake ni
ujinga, yeye atabaki kuwa kwenye orodha ya wabunge wa ajaabu ambao kila
siku kazi yake ni kumuwaza Kapunga badala ya kusimama na hoja.
“Mimi ninamsubili huku kwa wananchi,
sasa ngoja nimuache tu aendelee na utoto na jambo la kumsikitikia ni kwamba
mpaka leo anaamini akili za wanambea wa miaka mitano iliyopita ziko palepale,” alisema
Kwa hisani ya Mbeya leo blog
No comments:
Post a Comment