Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Marselin Mlelwa wakati wa akizungumza na wakulima wa Kijiji cha Idimi Kata ya Ihango wilayani hapa ikiwa ni maadhimisho ya siku ya wakulima. |
Mh. Diwani kata ya IhangoFosta Mwalingo akimkaribisha mgeni rasmi aongee na wakulima |
Ofisa kilimo wa Shirika la Mtandao wa Kilimo Hifadhi Barani Afrika (ACTN), Nicholaus Johaness, akitoa taarifa fupi kwa mgeni rasmi |
wakulima wa Kijiji cha Idimi Kata ya Ihango wilayani Mbeya wakimsikiiza mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wakulima. |
Evaristo Joshua Bwana shamba RUCCDIA akijibu moja ya maswali toka kwa wakulima wa Idimi |
Idi Abed bwana shamba toka YARA akitoa somo kwa wakulima |
Fadhili Katimba bwana shamba toka SYNGENTA akitoa somo kwa wakulima |
Wakulima wakipata somo katika shamba Darasa |
Ofisa kilimo wa Shirika la Mtandao wa Kilimo Hifadhi Barani Afrika (ACTN), Nicholaus Johaness, akitoa somo kwa wakulima katika shamba Darasa |
Mbeya. Wakulima wameshauriwa kulima mazao
mchanganyiko ya biashara na chakula ili kujiongezea kipato badala ya kuwa
na mtazamo wa zao la aina moja la mahindi au mpunga.
Rai hiyo ilitolewa juzi na Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Marselin Mlelwa wakati wa
akizungumza na wakulima wa Kijiji cha Idimi Kata ya Ihango wilayani hapa ikiwa
ni maadhimisho ya siku ya wakulima.
Mlelwa alisema ni muda mwafaka kwa wakulima
kubadili aina ya mazao wanayolima na kutazama mazao yenye fursa kubwa ya soko
tofauti na mahindi, maharage na mpunga.
“Sio lazima mkulima ung’ang’anie mahindi, mpunga
au maharage pekee kama zao la biashara wakati hivi sasa kuna mazao mengi kama
vile soya, ngano, ufuta na hata mihogo kwani yana soko kubwa na yanahimili pia
hali ya hewa” alisema mkurugenzi huyo.
Kwa upande wake, Ofisa kilimo wa Shirika la
Mtandao wa Kilimo Hifadhi Barani Afrika (ACTN), Nicholaus Johaness, alisema
wakulima wanatakiwa kutumia mbinu ya kilimo cha kubadilisha mazao katika shamba
moja ili kuendeleza rutuba katika ardhi na sio kulima zao la aina moja
kila mwaka.
Alisema wakulima wengi wamekuwa wakilima
na kupata mazao finyu kutokana na kulima zao la aina moja kila mwaka
katika hivyo ardhi kushindwa kuwa na rutuba nzuri.
Kwa upande wa wakulima walisema kilimo hifadhi
kimewasaidia wengi na kujiongezea kipato huku wakisisitiza kwamba kufuata
maelekezo ya wataalamu wa kilimo (maofisa ugani) inawasaidia kulima kwa kisasa
na kujipatia mazao mengi.
Mkulima wa kijiji hicho, Juma Mwasile
alisema ‘miaka ya nyuma tulikuwa tunalima tu bila kufuata mbinu bora kilimo
lakini hivi sasa baada ya kuanza kuwatumia maofisa ugani wengi wetu tumekuwa
tukipata mazao mengi” alisema Mwasile.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment