Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, March 2, 2015

TUKIO LA KUSIKITISHA: WAFANYAKAZI WA TANESCO MBEYA MKE NA MUME WAKUTWA WAMEKUFA NDANI YA NYUMBA YAO.

Baadhi ya majirani wa mtaa wa Hayanga RRM jijini Mbeya wakiwa nje ya nyumba ambapo tukio hilo limetokea .


Waombolezaji




Watu wawili wafanyakazi  shirika la Umeme Tanesco Mkoa wa Mbeya Ndugu Uswege Mwankuge (58) na Jusio Uswege (48) ambao ni mtu na mke wake wamekutwa wamekufa ndani ya nyumba yao mtaa hayanga  RRM jijini mbeya .


Tukio hilo la kusikitisha limetokea leo jijini hapa ambapo inadaiwa kuwa wawili hao wamekutwa wamekufa ndani ya nyumba yao usiku wa kuamkia leo Marchi 3 mwaka huu


Akizungumiza tukio hilo Balozi wa mtaa huo Jofrey Katuli amesema yeye alipigiwa simu majira ya saa 4 asubuhi  kuwa Ndugu Uswege Mwankuge pamoja na mke wake ndugu Jusio Uswege wamekufa wakiwa ndani ya nyumba yao  .


Amesema  watoto wa marehemu ndio waliogundua kuwepo   kuwepo kwa tukio hilo kutokana kuwepo kwa ukimywa wa muda mrefu ndani ya chumba cha wazazi wao ambapo walilazimika kuingia chumbani na kumkuta baba na mama yao tayari  wakiwa wamekufa .


Amesema baada ya kugonga kwa muda mrefu bila kufunguliwa walilazimika kubomoa mlango ambapo walikuta baba yao akiwa  amening'inia juu huku tayari akiwa amekufa kwa kujinyonga ambapo mama naye alikuwa amelala kitandani huku akiwa amekwisha fariki ambapo mwili wake ukiwa na majeraha shemu za usoni.

Amesema baada ya kupata maelezo hayo walipiga simu kituo cha Polisi ambapo walifika na kuchukua miili ya watu hao na kuipelekea hospital ya rufaa Mbeya  kwa ajiri ya uchunguzi zaidi.


 Kwa mujibu wa balozi huyo amedai kuwa inawezekana kuwa mwanaume huyo ambaye sasa ni marehemu  alimuua mke wake kwa kumpiga na kitu kizito kichwani hadi kufa kuku yeye akijaribu kujiua kwa kutumia sumu ambayo ilishindikana  na kutumia mbinu ya kujinyonga ambayo aklifanikiwa nayo.


Mmoja wa Majirani wa marehemu hao Ndugu Alex Kyabyara   amesema hawakuwahi kusikia ugomvi wa aina yeyote baina ya wawili hao  hivyo tukio hilo limewastaajabisha huku wakishindwa kujua nini chanzo cha mauji hayo.


Akithibisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa mbeya Ahmed Msangi amesema   tukio hilo limetokea majira ya saa Nne asubuhi ambapo amedai kuwa watu hao walikuwa na ungomvi usiku wa manane hali ambayo imepelekea mauiji hayo.


Aidha kamanda msangi amekili kuwa wawili hao ambao ni mke na mume bado walikuwa ni watumishi wa shirika la umeme tanesco mkoa wa mbeya hadi umauti huo unawakuta.


Amesema bado uchunguzi zaidi unaendelea kufanyika ili kubaini chanzo cha mauiji hayo ambapo miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika hospital ya rufaa jijini Mbeya.




JAMIIMOJA BLOG

No comments: