Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Saturday, March 14, 2015

DK, Nchimbi ahimiza wanawake kufuga ng’ombe wa maziwa

Mfugaji wa Ng'ombe wa maziwa Daina Mangula (Kulia), akimwelezea Mkuu wa Mkoa wa Njombe kuhusu faida za uzalishaji ikiwa ni pamoja na soko la mbegu za malisho ya mifugo.

Mkuu wa Wilaya ya Njombe,  Sarah Dumba akipata maelekezo ya mradi wa  Uendelezaji sekta ya maziwa Afrika Mashariki (EADD)  kutoka kwa maofisa wa mradi huo baada ya kutembelea banda la EADD.
Mkurugenzi Makaza wa Mradi wa Uendelezaji Sekta ya maziwa Afrika Mashariki, Mark Tsoxo akimwelewesha Mkuu wa Mkoa Dkt Rehema Nchimbi Kuhusu Mradi huo utakoa tekelezwa katika mikoa ya Njombe, Iringa na MbeyaMkuu wa mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi amewahimiza wanawake wa Njombe kuaangalia fursa za kujikwamua na umasikini.

Dk. Nchimbi alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani ambapo kwa mkoa huo yalifanyikia katika kijiji cha Ikuna wilayani Njombe.

Alisema ufugaji wa ng’ombe wa Maziwa ni chachu kubwa ya maendeleo mkoani Njombe, hivyo wafugaji wanaweza  kuwa na uhakika wa kupata chakula  pia inawapa fursa nyingi za biashara kama vile kuuza ,malisho ya Mifugo, Mbegu za Malisho na mbolea.

“Fursa hizi zikitumiwa vizuir zitakuza uchumi wa mkoa wa Njombe na Tanzania. Maziwa ya Njombe yanapendwa sana; imenifurahisha kujua kwamba msingi mkubwa wa ufugaji huu wa Njombe ni wanawake” alisema Dk. Nchimbi.

Alisema kwa Serikali na shirika la uendelezaji sekta ya Maziwa Afrika Mashariki (EADD) watafanya kazi na wafugaji wadogo wadogo, kuinua uzalishaji wa Maziwa Njombe ikiwemo pia kuwapa mafunzo kuhusu malisho, uhamilishaji na mafunzo ya biashara ili waweze kuongeza kipato.

Kwa upande wake, Ofisa mawasiliano wa mradi wa EADD nchini, Rachael Singo alisema  wanalenga zaidi kuwawezesha wanawake kwa lengo la kuonesha zaidi fursa za kiuchumi  ikiwa ni moja ya njia ya kuwaonesha wadau  nafasi ya mwanamke katika suala zima la kukuza uchumi kwa kaya na jamii kwa ujumla.


Alisema EADD  itaendelea kushirikiana na Serikali katika juhudi za kuondoa umaskini, kuondoa baa la njaa, uhakika wa kupata chakula cha kutosha na ustawi endelevu wa wananchi na kujiongezea kipato kwa njia ya kushiriki kazi za uzalishaji  wa maziwa.

Singo alisema mradi huo ambao utatekelezwa ndani ya miaka mitano, unalenga Kufikia kaya 35,000 za wafugaji wa ng’ombe wa maziwa  katika Nyanda za Juu Kusini kwenye mikoa ya Iringa, Njombe na Mbeya, ambapo asilimia 30 ya wafugaji hao ni wanawake .Kupitia Mnyororo wa thamani wa uzalishaji wa Maziwa ; wafugaji watapata fursa nyingi za biashara kwenye vitovu vya Maziwa chini ya mradi wa EADD”

Naye Afisa wa Maendeleo ya Jamii na Jinsia wa Mradi wa EADD, Lightness Munisi alisema mwanamke ni mdau mkubwa wa maendeleo katika jamii, hasa kwenye shughuli za ufugaji , hivyo siku ya wanawake duniani wanaitumia kuwahamasisha wanawake  kutambua fursa za kiuchumi zitokanazo na ufugaji wa kisasa wa ng’ombe wa maziwa ili  kuondokana na dhana ya utegemezi.

Mradi wa Uendelezaji Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki(EADD)  ; ni mradi unaotekelezwa na shirika la Mitamba Duniani ( Heifer International ) kwa kushirikiana na shirika la International Livestock Research  Institute (ILRI), TechnoServe,  ABS na World Agroforestry Centre. Mradi huu unawapa wafugaji fursa ya kujikwamua kimaisha kupitia mnyororo wa thamani wa maziwa

Mwisho.

No comments: