Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, February 5, 2015

WATUMISHI WA MAHAKAMA WAMETAKIWA KUWA NA WELEDI
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Noel Chocha akikagua gwaride

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Noel Chocha akitoa hotuba katika sherehe za Siku ya Sheria zilizofanyika katika ukumbi wa Mahakama kuu Kanda ya Mbeya

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akitoa neno la shukrani katika sherehe za Siku ya Sheria zilizofanyika katika ukumbi wa Mahakama kuu Kanda ya Mbeya.

Mwakilishi wa Mwanasheria wa Serikali Mfawidhi Kanda ya Mbeya, Archiles Mulisa akitoa mada  katika sherehe za Siku ya Sheria zilizofanyika katika ukumbi wa Mahakama kuu Kanda ya Mbeya.

Mwenyekiti wa Tanganyika Law Society(TLS) Mbeya, Joyce Kasebwa akitoa mada katika sherehe za Siku ya Sheria zilizofanyika katika ukumbi wa Mahakama kuu Kanda ya Mbeya.


Mwakilishi wa Shehe wa Mkoa, Shehe Abdalah Yondu akitoa sala  katika sherehe za Siku ya Sheria zilizofanyika katika ukumbi wa Mahakama kuu Kanda ya Mbeya.

.Mchungaji Frola akitoa maombezi katika sherehe hizo.Kwaya ya Mahakama kuu kanda ya Mbeya ikitoa burudani katika sherehe hizo.

Baby TOT

WADAU wa Mahakama wametakiwa  kuzingatia weledi na maadili ya kazi zao ili kutokuwa kikwazo kwa raia kupata fursa ya kuifikia haki yao.

Wito huo ulitolewa  na Mwakilishi wa Mwanasheria wa Serikali mfawidhi Kanda ya Mbeya, Archiles Mulisa alipokuwa akitoa mada kuhusu siku ya sheria katika  maadhimisho ya kuashiria kuanza kwa mwaka  mpya  wa shughuli  za Mahakama  ya Tanzania, maarufu kama siku  ya sheria ( law day) yaliyofanyika katika ukumbi wa Mahakama kuu kanda ya Mbeya.

Mulisa alisema Fursa ya kupata haki ipo katika mashauri ya jinai na yale ya madai hivyo  ili kuwa na fursa ya kupata haki ni lazima mamlaka za serikali, mahakama na wadau watimize wajibu wake ipasavyo na kuongeza kuwa pasipo kufanya hivyo haki haitapatikana kwa wananchi na hivyo kujenga jamii yenye manung’uniko dhidi ya serikali.

Alisema ni Wajibu wa serikali kuhakikisha kuwa taasisi zake zinazojihusisha na utoaji wa haki zinatekeleza majukumu yake kwa weledi na kwa misingi ya haki ili raia wake wawe na fursa ya kupata wanayostahili kwa mujibu wa sheria.


Aliongeza kuwa Mahakama ambayo ndicho chombo cha mwisho katika kutafsiri sheria na kutoa haki kina wajibu mkubwa pia wa kuhakikisha kuwa wananchi wanapata fursa ya kupata haki.


“ Kimsingi katika kutoa fursa kwa raia  kupata haki  Mahakama ina wajibu wa kutumia sheria zilizopo na kufanya tafsiri yake kwa ufasaha. Hali halisi sheria haziwezi kutaja kila kitu kinachoweza kutokea hivyo ni Mahakama zinazoamua kwa njia ya kulinganisha kesi, sheria na maamuzi ya mahakama yaliyotangulia” alisema Mwanasheria huyo.


Naye Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ambaye pia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Mbeya, Jaji Noel Chocha, alisema lengo la maadhimisho hayo ni kuashiria kuanza kwa mwaka mpya wa shughuli za mahakama nchini.

Alisema maadhimisho hayo hubebwa na kaulimbiu ambayo husema “fursa ya kupata haki wajibu wa serikali, mahakama na wadau” ambapo alisema sambamba na hilo huendesha maombi maalumu kutoka kwa viongozi wa dini ili shughuli zitakazofanyika ziwe kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu.

Aliongeza kuwa mwaka 2015 ni mwaka wenye matukio mengi na makubwa yanayolikabili taifa hivyo Mahakama inatambua kuwa uwezo wa kuyafikia hayo haiwezekani kwa utashi wa kibinadamu isipokuwa kwa uwezo wa Mwenezi Mungu kupitia maombi ya viongozi wa dini.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, ambaye alikuwa Mgeni wa heshima katika salamu zake, alisema Wananchi wanapaswa kutambua kuwa haki inayotakiwa kutolewa kwa wananchi ina gharama zake ambazo wahusika wanazichangia.

Alisema gharama ambazo mwananchi anapaswa kuchangia ili haki zake ziweze kupatikana ni kutii sheria jambo ambalo litasaidia kupunguza mlundikano wa kesi mahakamani na kuipunguzia serikali mzigo wa kufuatilia mambo ambayo hayakupaswa kufanyika endapo utii wa sheria ungezingatiwa.

Mwisho.
Na Mbeya yetu

No comments: