WADAU wa sanaa
ndani na nje ya mkoa wa Mbeya wameombwa kutoa ushirikiano kwa wasanii wa filamu
mkoani hapa kwa kununua kazi zinazofanywa na kuacha kasumba kuwa filamu bora
zinaweza kutengenezwa na wasanii walioko Dra es salaam pekee.
Mwongozaji wa
filamu wa kampuni ya Pritauj Filim Prince Hekela alitoa rai hiyo jana alipokuwa
akitambulisha Filamu mpya ya Vanilla iliyochezwa na wasanii kutoka mkoani
Mbeya.
Prince Hekela
alisema kumekuwa na kasumba ya baadhi ya wadau kuamini filamu nzuri ni zile
zinazochezwa na wasanii wa Dar es salaam jambo alilosema limekuwa likididimiza
sana wasanii wa mikoani.
Alisema ni
wakati kwa wadau hao kutambua kuwa ubora wa filamu hautokanani na mahali
anakofanyia kazi zake msanii,bali umakini na maandalizo bora ndiyo msingi wa
kutengenezwa kwa filamu bora.
Akizungumzia
filamu ya Vanila aliyosema tayari imeingizwa sokoni,alisema imeandaliwa katika
mazingira yenye kuzingatia staha hivyo haina vipande vyenye kuonesha aibu kiasi
cha familia kushindwa kuitazama kwa pamoja.
“Vanilla ni
filamu ambayo hata ukienda kuonesha uwanjani hakuna kinachozuia.Kwa nyumbani
hata awepo baba mama na watoto wanaweza kuiangalia kwa pamoja.Na ina mafundisho
ya kila mtu kulinagana na umri wake”
“Muhimu pia
wadau watambue kuwa tumejipanga kuhakikisha tunaleta burudani nzuri kutokana na
filamu zetu.Ndiyo sababu hata katika Vanila utaona tumechanganya wasanii wapya
na wa zamani.Wasanii wapya ambao wamefanya vizuri sana katika filamu hii ni
pamoja na Issa Ngoda,Regina Mwinyi, Kelvin Kaziyandege na Joachim Nyambo.Lakini
pia tumemshirikisha mwanadada Riyama Ally ambaye ni mkongwe katika sanaa”
alisisitiza Hekela.
Kwa upande wake
mmoja wa wasanii waliocheza filamu ya Vanila Joachim Nyambo alisisitiza kuwa
filamu hiyo imekuja kuwadhihirishia wadau kuwa kazi nzuri ya sanaa inaweza pia
kufanyika mikoani.
Nyambo aliwasihi
wadau kuendelea kushirikiana na wasanii mikoani wanaoonekana kukuza sanaa kwa
kuwa michango ya hali na mali ili kuwezesha kukua kwa sanaa.
|
No comments:
Post a Comment