Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, February 4, 2015

WASANII WA FILAMU MKOANI MBEYA WAANZA KUUZA FILAMU ZAO, FILAMU YA VANILA YAINGIZWA SOKONI.



WADAU wa sanaa ndani na nje ya mkoa wa Mbeya wameombwa kutoa ushirikiano kwa wasanii wa filamu mkoani hapa kwa kununua kazi zinazofanywa na kuacha kasumba kuwa filamu bora zinaweza kutengenezwa na wasanii walioko Dra es salaam pekee.

Mwongozaji wa filamu wa kampuni ya Pritauj Filim Prince Hekela alitoa rai hiyo jana alipokuwa akitambulisha Filamu mpya ya Vanilla iliyochezwa na wasanii kutoka mkoani Mbeya.

Prince Hekela alisema kumekuwa na kasumba ya baadhi ya wadau kuamini filamu nzuri ni zile zinazochezwa na wasanii wa Dar es salaam jambo alilosema limekuwa likididimiza sana wasanii wa mikoani.

Alisema ni wakati kwa wadau hao kutambua kuwa ubora wa filamu hautokanani na mahali anakofanyia kazi zake msanii,bali umakini na maandalizo bora ndiyo msingi wa kutengenezwa kwa filamu bora.

Akizungumzia filamu ya Vanila aliyosema tayari imeingizwa sokoni,alisema imeandaliwa katika mazingira yenye kuzingatia staha hivyo haina vipande vyenye kuonesha aibu kiasi cha familia kushindwa kuitazama kwa pamoja.

“Vanilla ni filamu ambayo hata ukienda kuonesha uwanjani hakuna kinachozuia.Kwa nyumbani hata awepo baba mama na watoto wanaweza kuiangalia kwa pamoja.Na ina mafundisho ya kila mtu kulinagana na umri wake”

“Muhimu pia wadau watambue kuwa tumejipanga kuhakikisha tunaleta burudani nzuri kutokana na filamu zetu.Ndiyo sababu hata katika Vanila utaona tumechanganya wasanii wapya na wa zamani.Wasanii wapya ambao wamefanya vizuri sana katika filamu hii ni pamoja na Issa Ngoda,Regina Mwinyi, Kelvin Kaziyandege na Joachim Nyambo.Lakini pia tumemshirikisha mwanadada Riyama Ally ambaye ni mkongwe katika sanaa” alisisitiza Hekela.

Kwa upande wake mmoja wa wasanii waliocheza filamu ya Vanila Joachim Nyambo alisisitiza kuwa filamu hiyo imekuja kuwadhihirishia wadau kuwa kazi nzuri ya sanaa inaweza pia kufanyika mikoani.

Nyambo aliwasihi wadau kuendelea kushirikiana na wasanii mikoani wanaoonekana kukuza sanaa kwa kuwa michango ya hali na mali ili kuwezesha kukua kwa sanaa.






No comments: