Mr. Sugu akiwa Hospitali.
Mbunge wa
Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi akifanya mawasiliano kwa ndugu
na jamaa mara baada ya kupata ajali mbaya na kunusurika kifo,ajali hiyo
imetokea eneo la Mlima Kitonga Mkoani Iringa mchana wa leo.kwa mujibu wa
chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa Mh. Mbilinyi alikuwa safarini
akitokea Mkoani Mbeya kuelekea jijini Dar akiwa na jamaa zake Wanne
katika gari hilo lenye namba za usajili T 148 BQE. katika ajali hiyo
hakuna aliyepoteza maisha.
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi (watatu kushoto) akizungumza namna hali ilivyokuwa mpaka kupata ajali hiyo.
Gari hiyo inavyoonekana.
Picha kwa hisani ya SufianiMafoto.com
No comments:
Post a Comment