Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, January 21, 2015

WAFANYABIASHARA MBEYA WAZUA TAFRANI, WAANDAMANA MAHAKAMANI WAKISHINIKIZA MWENYEKITI WAO AACHIWE


Wafanyabiashara  wanaondesha shughuli zao za kibiashara katika masoko zaidi ya  matano yaliyopo Jijini Mbeya, wakiwa nje ya mahakama ya Mwanzo ya Mbeya mjini, wakishinikiza mahakama hiyo kumuachia huru, Mwenyekiti wa Soko la Soweto  Honola Mbogella ambaye alifikishwa mahakamani hapo na halmashauri ya jiji la Mbeya kwa tuhuma za kuzuia watumishi wa umma kufanya kazi zao.


MWENYEKITI wa Soko la Sowetojijini Mbeya,  Honola Mbogella, amefikishwakatika  mahakama ya Mwanzo Mbeya mjinikwa tuhuma za kuzuia watumishi wa umma kufanya kazi zao.

 Kufuatia kukamatwa kwaMwenyekiti huyo kulisababisha zaidi  yawafanyabiashara 1000 wanaondesha shughuli zao za kibiashara katika masokomatano yaliyopo Jijini Mbeya, kuandamana na kuizunguka mahakama ya Mwanzo yaMbeya mjini, wakishinikiza mahakama hiyo kumuachia huru.

Mwenyekiti huyo,amefikishwa  katika mahakama ya Mwanzo yaMbeya mjini, leo na kesi yake kusikilizwa majira ya saa tatu asubuhi  ambapo kesi hiyo ilivuta hisia za watukutokana na kundi hilo la wafanyabiashara kuizunguka mahakama hiyo, huku jeshila polisi likilazimika kuimarisha ulinzi.

 Akisomewa mashitaka hayo Mbele  ya Hakimu wa Mahakama ya mwanzo ya Mbeya MjiniUbaswege Mathew, karani wa Mahakama hiyo, Sioni Kasunga, alisema mtuhumiwa huyoalifanya kosa hilo January 10 mwaka huu akiwa katika eneo lake la kazi la Sokola
Soweto lililopo Jijini Mbeya. Alisema, kwa mujibu wa kifungu kidogocha  cha sheria namba 101(a) sura ya 288iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, mtuhumiwa aliwazuia watumishi wa umma wahalmashauri ya Jiji la Mbeya kufanya kazi yao ya kukusanya ushuru.

 Alisema, mtuhumiwa aliwazuiawafanyabiashara hao  kugoma kutozwaushuru wa shilingi 200 hadi 300 na halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa maelezokwamba  licha ya wafanyabiashara hao kulipiatozo hiyo kwa kipindi kirefu bado soko hilo limeendelea kukithiri kwa uchafu.

 Aidha, kutokana na kosa hilo,Hakimu wa mahakama hiyo, Ubaswege Mathew,baada ya kusikiliza maelezo hayo,alitoanafasi kwa mtuhumiwa ambaye alikana shitaka hilo hivyo, hakimu kuhairisha kesi hiyo mpaka kesho na kwamba dhamana kwa  mtuhumiwa ipo wazi.

 “Kesi  hii nimeihairisha mpaka kesho  asubuhi, mtuhumiwa anahaki ya kuwekewadhamana kwa masharti ya kiasi cha fedha cha shilingi milioni mbili na wadhaminiwawili mmoja akiwa ni mtumishi wa
serikali,”alisema Wakati kesi hiyo ikiendeleamahakamani hapo, umati mkubwa wa wafanyabiashara wanaoendesha shughuli zaokatika masoko matano ya Soweto,Uyole, Mabatini, Sokomatola na Uhindiniulijitokeza na kuizunguka mahakama hiyo kwa kile walichokidai kwamba   Mwenyekityi huyo ameonewa. 

Wakizungumza naMbeya yetu ,nje ya mahakama, wafanyabiashara hao ambao waligoma kutaja majina yao, walisemawao wamegoma kulipa ushuru huo kutokana na halmashauri kushindwa kuetekelezamajukumu yao ya ukarabati wa miundombinu pamoja na usafi wa mazingira hivyoMwenyekiti huyo hausiki na  suala lakuwashawishi kugoma kama inavyodaiwa na halmashauri.

  Hata hivyo, wafanyabiashara haowamegoma kuendelea na shughuli zao mpaka suala hilo litakapo patiwa ufumbuzikwa halmashauri kurekebisha miundombinu na usafi wa mazingira katika maeneo yabiashara.
Mwisho. 
Na Mbeya yetu
   

2 comments:

Anonymous said...

Wamefanya vema sana wafanyabiashara kuandamana. Usafi ni jambo la msingi sana na daima maandamano huleta maendeleo na mabadiliko sehemu nying. Well done.

MASHAKA S.MBUGI said...

Kwa hatua ya uongozi wa jiji kuchukua hatua za kumshitaki kiongozi wa soko kutokana na madaiya uchafu uliokithiri sokoni hapo ni ukandamizaji uliokithiri na usiovumilika haswa ukizingatia ushuru wa sokoni sokoni hulipwa na wahusika ikiwa ni sehemu ya gharama za uendeshaji wa soko hilo ikijumuisha usafi unaofanywa na halmashauri. ninadhani imefika mahali mheshimiwa Rais Kama meuzi wa nafasi hizi kuangalia upya wateule wake na chama pia kuangalia upya madiwani na mameya wasijua wajibu wao, na namna wanavyopokea maoni ya wananchi na wadau mbalimbali.