Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, December 4, 2014

KARIBU KATIKA MAHAFALI YA 49 CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA (CBE), MBEYA YATAKAYO FANYIKA JUMAMOSI 6.12.2014 VIWANJA VYA MBEYA HOTEL


 Mkuu wa Chuo cha CBE Kampasi ya Mbeya,Dionise Lwanga, akiwa ofisini kwake akiendelea na maandalizi ya Mahafali ya 49 ya Chuo hicho.
 Afisa Uhusiano wa CBE, Leonidas Tibanga,akiendelea na majukumu yake kuhakikisha Mahafali ya 49 ya Chuo hicho yanafanikiwa.
 Baadhi ya Viongozi wakiendelea na kikao cha maandalizi ya Mahafali ya 49 ya CBE Kampasi ya Mbeya Jumamosi.
*******
MKUU wa Chuo cha Elimu ya Biashara (College of Business Education( CBE) Kampasi ya Mbeya,Dionise Lwanga, anawakaribisha wananchi wote katika Mahafali ya 49 ya Chuo cha CBE na Uzinduzi rasmi wa Kampasi ya Mbeya.
 
Sherehe za mahafali hayo zitafanyika Jumamosi Disemba 6, 2014 katika Viwanja vya Mbeya Hotel  zikitanguliwa na Uzinduzi wa Kampasi ambayo ofisi zake ziko katika majengo ya Chuo Kikuu Huria Forest ya Zamani Jijini Mbeya.
 
Mgeni rasmi katika Mahafali hayo ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdalah Kigoda.
 
Lwanga anasema siku hiyo itaanza na uzinduzi wa Kampasi kuanzia majira ya saa nne asubuhi Chuoni Forest ya zamani kisha mgeni rasmi atatembelea eneo la Chuo lililopo Iganzo na baadaye kuanza zoezi la kuwatunuku Wahitimu Mbeya Hotel.
 
Nyote mnakaribishwa!


No comments: