Bwana Rogers akiongozana na baadhi ya viongozi wa mtaa kwenda kituo cha polisi
Mwanamke
mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Juliana Josia(22)amezua utata hivi karibuni
baada ya kugunduliwa akishi na wanaume wawili kwa muda wa miaka minane bila
wanaume hao wawili kujitambua.
Hayo
yalibainika katika kituo cha Polisi Kati Jijini Mbeya baada ya Mwanamke huyo
kudai kuporwa mtoto mgogoni jinsi ya kike mwenye umri wa miaka miwili eneo la
Mwanjelwa Jijini Mbeya baada ya kutishiwa na Biton Bomani Mwashilindi mkazi wa
Ilemi Jijini Mbeya.
Juliana
alidai kuporwa mtoto na Biton Oktoba 27 mwaka huu majira ya saa nne asubuhi
alipokuwa akielekea soko la Sido kwenye shughuli zake za biashara na kutoa
taarifa kituo cha Polisi Mwanjelwa na baadaye kituo kikuu kati na kufunguliwa
jalada la wizi wa mtoto namba MB/RB/9384/2014 ambapo juhudi za kumtafuta
zilifanikiwa baada ya taarifa kutolewa Kituo cha Radio cha Bomba FM Mbeya ndipo
alipojisalimisha mwenyewe akiwa na mtoto Zalida Rogers(2).
Hata
hivyo katika hali ya mshangao Biton alifika katika kituo cha Polisi Kati akiwa
na Cheti cha kuzaliwa na kadi ya kliniki ambapo kinaonesha mtoto Zalida
kuzaliwa kituo cha Afya Ruanda Mwanjelwa na kuonesha kuzaliwa 18/08/2012 wazazi
wakiwa ni Juliana Josia na Biton Mwashilindi.
Biton
alidai mbele ya Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi kuwa Juliana ni mpenzi wake
kwa muda wa miaka nane na kwamba walikuwa wakikutana katika nyumba ya kulala
wageni kila alipomhitaji na walikuwa wakipanga katika nyumba hiyo kwa siku saba
kila wanapokutana hali ilyofanya watu wanaosikiliza tukio hilo kituo cha Polisi
kushikwa na butwaa akiwemo mume halali Rogers Halinga na mke wa Biton ambaye
alimtunza mtoto kwa siku nne.
Akijieleza
kwa kujiamini Biton alidai kuwa hata mtaji wa biashara alimpatia yeye na hata
wazazi wake Biton walioko Itaka Mbozi walimtambua mtoto Zalida na kwamba jina
la mtoto alipewa na ndugu zake na hata aliowahi kuugua alikwenda Itaka Mbozi na
kukaa kwa wazazi wa Biton kwa zaidi ya juma moja.
Kwa
upande wa Rogers yeye alisema mtoto Zalida ni wa kwake na kwamba aliondoka kwao
akiwana na ujauzito wa miezi mitano na kwamba yeye alijua kukorofishana kwao
kulitokana na hali ya ujauzito na alikaa kwamba mkewe Juliana alikaa kwao
kwa miezi sita na alipojifungua alirejea kwake na aliohitaji kupata maendeleo
ya mtoto mkewe alidai kuwa kadi ya kliniki imepotea.
Kikao
hicho kilichokuwa na mvutano mkubwa kiliahirishwa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya
Mbeya kwa kumshikilia Biton kwa kosa la kutorosha mtoto na kesi ya ugoni na
kuwa atafikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika huku Rogers
akikabidhiwa mkewe na mtoto kwa minjili ya kwenda kuyajenga huko nyumbani kwao
Kijiji cha Ishungu Kata ya Ruiwa wilaya ya Mbarali.
Baba
mzazi wa Rogers Mzee Jason Halinga alisema alishangazwa na kitendo kilichofanwya
na mwanamke huyo ambapo alidai kuwa mwanae alioa kihalali na kufuata mila zote
na kulipa mahari lakini alishangazwa na kitendo cha wazazi wa Juliana kushindwa
kuonesha ushirikiano hali inayoashiria kujua kile kilichokuwa kinafanywa na
mtoto wao.
Biton
alifika kituo cha Polisi akiwa na mkewe wa ndoa ambapo naye hakufahamu kuwa
mumewe anaishi na mke mwingine nje ya ndoa na kwamba mtoto Zalida alipoletwa
kwake hakuambiwa chochote kile na kwamba ameishi kwenye mateso ya ndoa kwa muda
wa miaka nane huku akifanyiwa vitendo vya kikatili na mumewe ikwa pamoja na
kuambulia kipigo mara kwa mara.
Baadhi
ya ndugu wa Rogers walioneshwa kukerwa na baadhi ya Askari wa ngazi juu
katika Dawati la Jinsia Kituoni hapo ambao walonesha kutojali suala hili huku
wakitioa maneno ya kejeli hali inayotia dosari utendaji kazi wa Dawati hilo na
kwamba lipo kibiashara zaidi na si huduma kama ilivyo sera ya Jeshi la
Polisi.
Hata
hivyo hawakusita kuwapongeza Askari wa Kiume walionesha juhudi hata kufanikwa
kupatikana kwa mtoto Zalida na Biton pamoja na rafiki yake.
Katika
sakata hili kama si juhudi za Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi
kuingila kati basi mtoto Zalida asingeweza kupatikana kama baadhi ya watoto
waliotoweka maeneo mbalimbali Mkoani Mbeya ambao hawajapatikana mpaka sasa
ambapo wananchi wamelalamikia Kituo Kikuu cha Kati kwa kutochukua hatua za
haraka za kukomesha vitendo vya ukatili wa Kijinsia na baadhi kuamua kumalizana
wenyewe mitaani vikiwemo vitendo vya ubakaji ambavyo vimeshamiri mkoani Mbeya.
Hatima
ya ndoa ya Rogers na Juliana itajulikana baada ya mazungumzo yatayofanyika kwa
Mzee Jason Halinga nyumbani kwake Ishungu Kata ya Ruiwa hivi karibuni kikao
kitakutaniha pande mbili za wazai ili kufikia muafaka katika sakata la aina
yake na kwamba hata kubainika kwa sula hili ni kutokana na Juliana kufumwa na
mwanaume mwingine katika chumba ambacho Biton alikuwa awe na Juliana ndipo
alipoamua kulipiza kisasi kwa kutorosha mtoto.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment