Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, November 30, 2014

MAHAFARI YA 12 YA TIA MBEYA YAFANA, WAHITIMU NA WAHADHIRI WAPEWA SOMO.

Mgeni rasmi wa Mahafari ya 12 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania(TIA),Profesa Norman Sigalla King ambaye alimwakilisha Waziri wa Fedha, Saada Salum Mkuya akiwatunuku vyeti wahitimu.

Mgeni rasmi na viongozi wengine wakiwa meza kuu katika mahafari ya 12 ya TIA.

Afisa Mtendaji mkuu wa TIA, Dk. Joseph Kihanda akitoa taarifa ya chuo katika mahafari ya 12 ya TIA kampasi ya Mbeya

Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya Wizara ya Fedha, Profesa Isaya Jairo, akimkaribisha mgeni rasmi kutunuku vyeti kwa wahitimu katika mahafari ya 12 ya TIA Kampasi ya Mbeya.


wahitimu wakitunukiwa vyeti kulingana na fani walizosomea. Maandamano.


 Mgeni rasmi akiwa kwenye maandamano.


Brass band ikiongoza maandamano


Vikundi mbalimbali vya ngoma vilitumbuiza katika Mahafali hiyo

WAHADHIRI wa Vyuo mbali mbali nchini wametakiwa kutoa elimu kwa wanafunzi kulingana na soko la ajira ikiwa ni pamoja na fani inayoendana na cheti alichopata ili kukabiliana na changamoto zinazojitokeza.

Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Profesa Norman Sigalla, alipokuwa amemwakilisha Waziri wa Fedha, Saada Salum Mkuya, katika mahafali ya 12 ya Taasisi ya Uhasibu (TIA)Kampasi ya Mbeya yaliyofanyika katika viwanja vya taasisi hiyo mjini hapa.

Profesa Sigalla alisema hivi sasa kuna ushindani wa vyuo na ukosefu wa ajira nchini hivyo I vema wahadhiri wakatoa wanafunzi wenye sifa kulingana na vyeti wanavyopata ili kukidhi soko la ajira ikiwa ni pamoja na kujiajiri wenyewe na sio kusubiri kuajiriwa.

“ kutokana na ongezeko la vyuo na ushindani uliopo ni vema wahadhili wakatoa wahitimu wenye sifa za kipekee kuendana na aina ya cheti alichopata na kukabiliana na soko la ajira” alisema Profesa Sigalla.

Aliongeza kuwa wajibu wa vyuo ni kuandaa watalaam mbali mbali ili waweze kutumikia taifa na kukidhi haja ya nchi katika kujiletea maendeleo kwa wahitimu kufuata walitofundishwa madarasani na kutumia taaluma yao kupambana na changamoto zilizopo uraiani.

Alisema ni vema wahitimu kutokana na elimu waliyoipata wakaangalia fursa zilizopo nchini wakazitumia vizuri badala ya kusubiri kuajiriwa na serikali kutokana na mfumo uliopo wa kutoa ajira kwa kila mtu kuwa mgumu baada ya wahitimu kuongezeka kila kukicha.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji mkuu wa Tasisi ya Uhasibu Tanzania(TIA) Dk. Joseph Kihanda,alisema katika mwaka wa masomo 2013/2014 jumla ya wanafunzi 1960 wakiwemo wanawake 947 na wanaume 1013 wamehitimu katika fani za cheti cha awali, Stashahada na stashahada ya uzamili katika kampasi ya Mbeya.

Alisema Chuo hicho kinakabiliwa na Changamoto za kudumu na mpya ambazo ni uhaba wa majengo kama vile kumbi za mhadhara, maktaba za kisasa na vitabu, ofisi za wafanyakazi na nyumba za wafanyakazi na wahadhiri pamoja na upungufu wa thamani.

Aliongeza kuwa changamoto mpya zinazokikabili chuo hicho ni pamoja na uwiano wa wahadhirina wanafunzi kutokuwa mzuri kutokana na ongezeko kubwa la udahili kutokana na ajira ya wahadhiri kusimamiwa na Serikali kuu hivyo kushindwa kupata wahadhiri wanaoweza kuendana na idadi wa wanafunzi  ambapo hivi sasa chuo kina wahadhiri 19.

Dk Kihanda aliongeza kuwa Changamoto  nyingine ni upatikanaji wa maji katika Kampasi ya Mbeya kuwa ni wa kusuasua hivyo kuhatarisha afya za wanafunzi kunakoweza kusababishwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi inayofikia 3007.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi,Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya Wizara ya Fedha,Profesa Isaya Jairo, alisema kazi ya bodi ya ushauri ni kutoa ushauri ili kuendeleza jitihada za serikali katika kutekeleza malengo makuu ya taasisi.

Aliyataja malengo ya taasisi kuwa ni kutoa mafunzo, kufanya tafiti na kutoa ushauri kwenye fani za uhasibu, ununuzi na ugavi, uongozi wa biashara, usimamizi wa rasilimali watu, masoko na uhusianowa jamii pamoja nauhasibu wa fedha za umma na katika Nyanja nyingine za biashara.

Mwisho.

                                               Na Mbeya yetu

No comments: