Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, October 10, 2014

VITUKO MITAANI NANI ALAUMIWE KATI YA JIJI NA TANESCO MBEYA KWA KITUKO HIKI

Hii hatari kwa waendesha magari nyakati za usiku hii nguzo ipo barabara mpya jirani ya bustani ya jiji eneo la uwanja wa sokoine jijini Mbeya 
Je? ushirikiano wa Halmashauri ya jiji la Mbeya na Tanesco hakuna mmeshindwa kukaa chini mkajadili swala hili maana yote mnayofanya ni kwafaida ya wananchi 
Picha yenyewe inajieleza je mnasubiri ajali itokee ndiyo mchukue hatua?
Hii hatari sana ujumbe tunaimani umefika 


Picha na Mbeya yetu

4 comments:

Anonymous said...

Mambo mengine watu wazima wanafanya ambayo hata mtoto wa miaka mitano hawezi kufanya jambo kama hili. Kweli wapi na wapi nguzo kati ya barabara jamani! kweli ni kichekesho na maudhi. Na wamwaga kokoto wameridhika wakamwaga Da! kazi kweli kweli. Anyway blog ya Mbeya yetu mko juu, na ninyi ndo mtakaosababisha maendeleo makubwa sana Jijini Mbeya ninawaombea sana.

Anonymous said...

People are not serious on the burning issues like these

Mjamii said...


Shida hawa mabwana ofisini kimya wamekaa, kila mmoja anazani sio jukumu lake katika kuona usahihi wa vitu. Hawa mabwana wa Tanesco wao wanafikili kwa hilo sio jukumu lao ila wao ni kukata umeme na kuwafungia watu umeme tu na hao ndungu wa jiji wao wanaona hilo sio jukumu lao wao ni kukusanya kodi na kukimbizana na wamachinga pia mmwaga kokoto yeye alifanya kile kilichoko katika makubaliana ya tenda kumwaga kokoto na kuchimba mitalo, ila naamini kabisa aliendelea kufanya kazi yake ya kumwaga kokote na pindi alipofika hapo aligundua hiyo tenda amepewa na WEHU! maana mtu mkamilifu angehakikisha kwanza hizo nguzo zimetoka kisha marekebisho ya barabara yafuate. Inasikitisha sana pindi unapogundua watu wengi maofisini hawako siliasi na majukumu yao.

Anonymous said...

Mbeya Blog,
Mnafanya kazi kubwa, muda si mrefu watakuja kuondoa hiyo mkanaganyiko wa mipango miji usiokubalika!
Big up Mbeya Blog.