Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, October 17, 2014

VISHALE (DARTS) MBEYA WAMUENZI BABA WATAIFA


Mwenyekiti wa Darts Mkoa wa Mbeya, Weston Asisya Siku hii ni muhimu kwetu hasa wapenda Michezo Amani na demokrasia. Na ndiyo maana tumekusanyika hapa sisi wacheza vishale (DARTS)  jiji la Mbeya kumuenzi baba wa taifa maana alikuwa mpenda michezo sana alisema hayo mwenyekiti Asisya hivi karibuni katika mashindano ya vishale kwa timu za Apple line, Magereza, polisi na Tumaini zote za jijini Mbeya

Mashindano ya vishale yakiendelea katika ukumbi wa Apple line jijini Mbeya


Raymond Mushi wa timu ya Apple Line akikabidhiwa kikombe na pesa taslim Sh  30,000/ kwa kunyakuwa ushindi wa kwanza katika shindalo hilo la kumuenzi  baba wa Taifa

Lazaro Kasenegala mshindi wa tatu akipokea kikombe na pesa taslimu 10,000/ toka kwa Mwenyekiti wa DARTS mkoa wa Mbeya

Hussen kutoka timu ya tumaini mshindi wa pili akipokea kikombe na pesa taslimu 20,000/ toka kwa Mwenyekiti wa DARTS Mkoa waMbeya

Picha ya washindi wakiwa na Mwenyekiti wa vishale mkoa wa Mbeya

Na Mbeya yetu

No comments: