Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, September 2, 2014

ZIARA YA UTALII WA NDANI SEHEMU YA PILI : MBEYA YETU BLOG WATEMBELEA MAPOROMOKO YA KAPOROGWE

Ilikuwa ni Moja ya Safari ambazo zilikuwa na Mafanikio Makubwa ambapo Tone Multimedia Group kupitia Mtandao wao wa Mbeya Yetu Blog tuliamua kuanza Rasmi kuvitangaza vivutio vya kitalii ambavyo tunaamini vimesahaurika kwa njia moja au yengine, katika Safari yetu ya kuvitangaza vivutio hivyo tumeanza moja kwa moja na Mkoa wa Mbeya.

Kwanza kabisa tulifika katika Kijungu na Kujionea mengi.. Kama ulikosa kuona juu ya kijungu Bofya hapa  MBEYA YETU ILIPOTEMBELEA KIJUNGU 

Leo katika mwendelezo wa vivutio hivyo vya Utalii katika Mkoa wa Mbeya tutakiangazia kivutio kimoja wapo ambacho ni Maporomoko ya Kaparogwe, Maporomoko haya ni moja ya Kivutio kikubwa cha Utalii Nchini Tanzania ambacho kinavutia sana. 

Maporomoko haya ambayo yapo Kilometa 11 kutoka Ushirika Tukuyu sehemu ambayo kuna barabara nzuri na Gari la aina yoyote inaweza kufika katika kivutio hicho.

Kikosi kazi cha Mbeya yetu tulifika eneo Hilo na kujionea wenyewe eneo hilo na kujionea Maliasili hii na eneo ambalo kwa hakika linahitajika kusapotiwa na kulitangaza ili Dunia ipate fahamu kuwa kuna eneo kama hilo na wanahitaji kufika na Kutembelea.

Hivi ndivyo Safari yetu ilivyokuwa.. Fuatilia hapa 

Unaweza ukastaajabu sana , Mto huu unaitwa Mto rangi kwa jina halisia , Jina la kaporogwe limekuja baada ya mtu mmoja aliyekuwa eneohili zamani za kale kudondoka katika maporomoko haya na Kuitwa Kaporogwe.  Maji haya ndiyo  yanaonekana yakitembea kwa kasi ndogo lakini ndiyo yanayoenda kumwaga maji yake katika maporomoko ya Kaporogwe.
Haya ndiyo Maporomoko ya Kaporogwe yanavyo onekana kwa ukaribu kabisa
 Hii ni njia yakuelekea Maporomoko ya Kaporogwe 
 Utalii wa ndani baadhi ya watu wanaelekea katika Maporomoko ya Kaporogwe
 Huu ni upande wa kuingilia kwa mbali ndivyo maporomoko yanavyo onekana 
 Kama kawaida unapotembelea maeneo kama haya lazima upate ukodaki wa kumbukumbu hapa kila mmoja akichukua matukio
Kwa hakika Joseph Mwaisango Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu akiwa mwenye furaha alipofika katika maporomoko haya ya kaporogwe mara baada ya kujionea yeye mwenyewe. Hapa ni eneo la Ndani kabisa ya Maporomoko hayo.
 Hili ni Moja ya eneo la Mapumziko, watu wanaofika huja hapa na kukaa kisha kutazama uzuri wa Maporomoko ya Kaporogwe 
 Maji yakiwa yanashuka kwa kasi katika maporomoko ya Kaporogwe 
 Kwa Jirani kabisa Maji yanavyomwagika katika Maporomoko ya kaporogwe 
 Unaweza ukaona maajabu sana lakini hii ndio njia ya kuingilia maporomoko ya kaporogwe 
Head of Group Research and Product Development wa Tone Multimedia Group ambao ni Wamiliki wa Mbeya yetu Blog Fredy Anthony Njeje akiwa chini kabisa ya Maporomoko ya Kaporogwe kujionea jinsi maji yanavyo mwagika, katika eneo hili la chini kuna hali ya unyevu vyavu na baridi ya aina yake ambayo haiumizi lakini inayohamasisha kuendelea kuwepo katika eneo hilo muda wote.
 Hii ni Barabara inayotokea eneo Linaitwa Kissa kuelekea katika Maporomoko ya Kaporogwe 
Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu Blog Joseph Mwaisango wa Kwanza kulia akiwa na wenyeji wanaokaa maeneo ya Maporomoko ya Kaporogwe.
 Wa kwanza kulia ni Fredy Anthony Njeje akiwa pamoja na wakazi wanaoishi maeneo ya Kaporogwe 
Hii ni Barabara nzuri ya Kuelekea katika maporomoko ya kaporogwe.

Imeandaliwa na Tone Multimedia Group kupitia Mtandao wake wa Mbeya yetu Blog ambao upo ndani ya Blogs za Mikoa. 

Je unapenda  kutoa maoni au kuungana nasi katika kampeni hii Piga simu ama tuma ujumbe mfupi wa maneno kupitia +255 765056399 au +255 754374408.


No comments: