UONGOZI wa Tone Multimedia Company
Ltd ambao ndiyo wamiliki wa Mtandao wa Blogs za Mikoa Tanzania www.blogszamikoa.blogspot.com ukiwemo wa Mbeya yetu www.mbeyayetu.blogspot.com
unapenda kuwataarifu wadau wake wote hususani Wahariri wa Magazeti na redio
mbali mbali za Mkoani Mbeya na nchini kuwa wanaposoma na kuchukua habari kwenye mitandao yetu
wajaribu kuandika au kutaja chanzo chake.
Tumelazimika kutoa taarifa hii
baada ya kuwepo kwa Vyombo vya habari vikubwa kuwa na tabia ya kukopi na
kutumia habari za kutoka Mbeya yetu
na Blogs zengine za Mikoa bila kutaja wapi walikoipata hiyo habari.
Kiukweli hali hiyo
inatusononosha kutoka na mazingira ambayo tunakuwa tumeyapata pindi
tunapofuatilia matukio mbali mbali ikiwemo kuhatarisha maisha na usalama pamoja
na gharama tuzitumiazo katika kufuatilia habari husika.
Aidha Mtandao wa Mbeya yetu haukatazi kwa Media yoyote
iwe nje au ndani ya nchi kutumia habari zetu na ndiyo maana hazijafungwa hivyo
ombi letu kwenu wadau ni kuandika chanzo chako cha habari ni wapi hiyo
inachangia sisi kuona wewe mdau wetu umetambua mchango wa Mbeya yetu.
Hata hivyo Uongozi pia unatoa
rai kwa Wahariri wa Vyombo vya habari nchini na Mkoa wa Mbeya kwa ujumla
kuthamini mchango wa vyombo vidogo na vya chini vinavyofanya kazi za kijamii
kama ilivyo kwa Mtandao wa Mbeya yetu.
Hivyo basi kwa mantiki hiyo,
Uongozi wa Mbeya yetu unapenda kuwataarifu hautasita kuwachukulia hatua za
kisheria wale wote watakaotumia taarifa
za Mbeya yetu na Blog za Mikoa zinazomilikiwa na Tone Multimedia bila kutaja chanzo chake.
Tunategemea ushirikiano kutoka
kwenu katika kuikomboa jamii ya Kitanzania na mahitaji walionayo na michango ya
vyombo vya habari kwa jamii husika.
Imetolewa na Uongozi wa Tone Multimedia Company Limited,
No comments:
Post a Comment