Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, September 22, 2014

WANANCHI WAONYWA KUSHABIKIA MAANDAMANO YA SIASA‏

 Meza kuu, viongozi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mbarali na Kata ya Chimala katika sherehe za kumtambulisha Kamanda wa Vijana (UVCCM) kwenye matawi ya chama hicho.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM, Leonard Kitalima akizungumza jambo kabla ya kumtambulisha Kamanda wa Vijana wa Kata ya Chimala.
  Kamanda wa vijana wa UVCCM Kata ya Chimala, Francis Mtega akifuatilia kwa makini sherehe za kumtambulisha kwenye matawi.
 Kamanda wa vijana wa UVCCM Kata ya Chimala, Francis Mtega akifungua jiwe la wakereketwa la UWT katika kilabu cha Songambele tawi la Mengele kwenye sherehe za kumtambulisha kwenye matawi.
 Kamanda wa vijana wa UVCCM Kata ya Chimala, Francis Mtega akipandisha bendera katika kijiwe cha wakereketwa cha Songambele tawi la Mengele  kwenye sherehe za kumtambulisha kwenye matawi.

baadhi ya Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakiwa kwenye sherehe za kumtambulisha Kamanda wa Vijana kata ya Chimala 



WANANCHI nchini wametakiwa kutii amri halali zinazotolewa na jeshi la Polisi ili kuepuka kujiingiza kwenye vurugu zisizokuwa na msingi wowote ikiwa ni pamoja na kutii utawala wa sheria bila shuruti.
Wito huo ulitolewa jana na Kamanda wa Umoja wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM), Kata ya Chimala wilayani Mbarali Mkoa wa Mbeya,Francis Mtega, wakati akitambulishwa kwenye matawi ya chama hicho.
Alisema kazi ya Wanasiasa ni kuwaelekeza wananchi namna ya kufanya kazi ili kupata maendeleo ili kuinua uchumi wao na sio kuwahamasisha kufanya maandamano na kukaidi amri halali za jeshi la polisi hali inayozua vurugu kwenye jamii na kurudisha maendeleo nyuma.
Aliongeza kuwa endapo kila mtu atakuwa akijishughulisha na kazi za maendeleo hakuna mwanasiasa atakayeweza kumshawishi kufanya maandamano wakati akijua atapoteza kipato kutoka kwenye biashara yake anayoifanya.
Alitolea mfano kwa umoja wa vijana kwamba ni taasisi kama zingine hivyo zinapaswa kujiunga kwenye vikundi na kubuni vitega uchumi mbali mbali ili kuweza kupata fedha kutoka kwenye Halmashauri ambazo hutenga asilimia 5 ya mapato kila mwaka kwa ajili ya kusaidia vijana.\
Mtega aliwaambia wananchi waliofurika katika mikutano ya utambulisho kuwa moja ya majukumu yake ni kuhakikisha Chama kinashinda katika chaguzi zake na kutoa wito kwa wananchi na wanachama kumuunga mkono ili kuwa na nguvu ya pamoja.
Katika utambulisho huo, Kamanda Mtega pia alizindua jiwe la wakereketwa wa Umoja wa Wanawake(UWT) eneo la Songambele na kusimika bendera katika Tawi la Mengele, Kilabu A na Kilabu B pamoja na tawi la Muala yote ya Kata ya Chimala.
Mbali na kufungua matawi hayo pia Kamanda huyo alioyeongozana na Madiwani wa Kata, Viti maalumu na Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi wa CCM wilaya ya Mbarali, Leonard Kitalima, walikabidhi kadi kwa wanachama wapya 170.
Sambamba na shughuli hiyo pia viongozi hao walishiriki harambee ya ujenzi wa choo katika Kilabu kinachoendeshwa na Umoja wa Wanawake tawi la Mengele kinachogharimu zaidi ya shilingi Milioni 1.8.
Aidha katika harambee hiyo jumla ya shilingi 570,000 zilipatikana, ahadi shilingi 650,000 na  kufanya jumla ya fedha zilizopatika kuwa Milioni 1.2 huku nguvu ikithaminiwa kufikia shilingi laki 5.
Na Mbeya yetu

No comments: