Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, September 24, 2014

MBEYA CITY YATAKIWA KUOMBA MECHI ZA KIRAFIKI NA TIMU ZA MALAWI.

Balozi wa Tanzania Nchini Malawi, Patrick Tsere, mwenye suti katikati akipokea picha ya ya wachezaji wa Mbeya City toka kwa wanahabari wa mkoa wa Mbeya




TIMU ya mpira wa miguu ya Mbeya City inayomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya imetakiwa kupeleka mwaliko wa kuomba Timu za kujipima nguvu  kutoka nchini Malawi ili kuimarisha ujirani mwema kupitia sekta ya michezo.

Hayo yalibainishwa na Balozi wa Tanzania Nchini Malawi, Patrick Tsere, alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari wa Mkoa wa Mbeya waliofanya ziara ya kimafunzo nchini Malawi na kumkabidhi picha ya Wachezaji wa Mbeya City kwa lengo la kuitangaza timu hiyo kimataifa.

Balozi Tsere alisema atalichukua jukumu la kuitangaza Mbeya City kama moja ya kazi yake nchini Malawi isipokuwa suala muhimu ni uongozi wa timu hiyo kutuma barua za maombi ya kuzialika timu kutoka Malawi ili kucheza michezo ya kirafiki hali ambayo itachangia kuimarisha ujirani mwema na ushirikiano uliopo.

Suala na kuinadi Mbeya City limetokana na maombi ya Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa waandishi wa Habari waliofika Ofisini kwake kumuaga katika safari ya kuelekea nchini Malawi ambapo alisema hivi sasa Mbeya city inajulikana kila kona nchini hivyo inabidi itangazwe kimataifa.

Hata hivyo Waandishi hao wakiwa nchini Malawi, mbali na kumkabidhi picha Balozi pia walipata kuzungumza na Waziri wa Habari, Utalii na utamaduni wa Malawi, Kondwani Nankhumwa, ambaye alipogusiwa kuhusiana na Mbeya city alisema haina tatizo atalifikisha kwa Afisa anayehusika na michezo.

Alisema mbali na kulifikisha suala hilo kwa afisa anayehusika pia alisema ni jukumu la Mbeya City kupeleka barua ya mwaliko kwani kuna timu nyingi ambazo zinaweza kupambana na Mbeya city katika michezo ya kirafiki.

Mwisho.

Na Mbeya yetu

        

1 comment:

Anonymous said...

Mbeya City na nyie mujenge uwanja wenu wa Mpira sio kung'ang'ania uwanja wa sokoine, mmekuwa juu kwa kiwango cha mpira iweni juu kwa maendeleo ya uwanja wenu kama Azam. Iwambi kule maeneo makubwa ya kutosha kujenga uwanja na ofisi zenu. Changamkeni