Picha kwa Hisani ya Father Kidevu Blog
Tone Multimedia Group ambao ni wamiliki wa Mtandao wa Blogs zamikoa Tanzania, Tone Radio-Tz, This Day Magazine na Matukio na wanavyuo, Tumepokea kwa masikitiko makubwa Taarifa za Ajali mbaya iliyotokea Musoma Ambayo ilihusisha Basi la J4 Express T677CYC lililokuwa linatoka Sirari kwenda Mwanza limegongana uso kwa uso na basi la Mwanza Coach T736AWJ Tarehe 5.09.2014 Majila ya Mchana katika eneo la sabasaba Musoma wakati moja ya mabasi hayo likiovateki basi lengine ambapo watu zaidi ya 39 wamepoteza maisha huku wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa. Mpaka sasa Maiti 25 zimetambuliwa kati ya 39 na ndugu wa Marehemu.
Tunaungana na watanzania wote kuwapa pole ndugu waliopotelewa na Ndugu, Jamaa na Marafiki waliopoteza ndugu zao katika ajali hii, Pia tunawapa pole wale Majeruhi wote Tunawaombea kwa Mungu wapate kupona Haraka ili tuje kuweza kuungana nao katika Kujenga Taifa.
Imetolewa na uongozi
Tone Multimedia Group
1 comment:
Kwa kweli inasikitisha sana. Madereva kuweni makini kwa sababu munashika vyombo vya moto jamani. Muogopeni Mungu kwa kuendesha magari hovyo hovyo. Askari wa usalama barabarani punguzeni rushwa na fanyeni kazi kuokoa jamii. Rushwa ni kitu cha kupita tu hakikupatii amani ya roho yako. Zaidi unasutwa tu nafsini mwako kupokea pesa isiyo harali na kuharalisha makosa. Muogopeni Mungu nanyi pia.
Post a Comment