Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, September 5, 2014

SALAM ZA RAMBI RAMBI KUTOKA TONE MULTIMEDIA GROUP KUTOKANA NA AJALI ILIYOTOKEA MUSOMA LEO.Picha kwa Hisani ya Father Kidevu Blog

Tone Multimedia Group ambao ni wamiliki wa Mtandao wa Blogs zamikoa Tanzania, Tone Radio-Tz, This Day Magazine na Matukio na wanavyuo, Tumepokea kwa masikitiko makubwa Taarifa za Ajali mbaya iliyotokea Musoma Ambayo ilihusisha  Basi la J4 Express  T677CYC lililokuwa linatoka Sirari kwenda Mwanza limegongana uso kwa uso na basi la Mwanza Coach T736AWJ  Tarehe 5.09.2014 Majila ya Mchana katika eneo la sabasaba Musoma wakati moja ya mabasi hayo likiovateki basi lengine  ambapo  watu zaidi ya 39 wamepoteza maisha huku wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa. Mpaka sasa Maiti 25 zimetambuliwa kati ya 39 na ndugu wa Marehemu.

Tunaungana na watanzania wote kuwapa pole ndugu waliopotelewa na Ndugu, Jamaa na Marafiki waliopoteza ndugu zao katika ajali hii, Pia tunawapa pole wale Majeruhi wote Tunawaombea kwa Mungu wapate kupona Haraka ili tuje kuweza kuungana nao katika Kujenga Taifa.

Imetolewa na uongozi
Tone Multimedia Group
1 comment:

Anonymous said...

Kwa kweli inasikitisha sana. Madereva kuweni makini kwa sababu munashika vyombo vya moto jamani. Muogopeni Mungu kwa kuendesha magari hovyo hovyo. Askari wa usalama barabarani punguzeni rushwa na fanyeni kazi kuokoa jamii. Rushwa ni kitu cha kupita tu hakikupatii amani ya roho yako. Zaidi unasutwa tu nafsini mwako kupokea pesa isiyo harali na kuharalisha makosa. Muogopeni Mungu nanyi pia.