Mgeni rasmi Patrick Zambi akiwa katika picha ya pamoja na Wachezaji wa Salalizya pamoja na zawadi zao baada ya kuibuka washindi wa kwanza.
TIMU ya Mpira wa Miguu kutoka Baa ya
Salalizya iliyopo Mabatini jijini Mbeya imeibuka kidedea katika Bonanza
lililoshirikisha Timu za Mabaa lililoandaliwa na Serengeti fiesta maarufu kwa
jina la Serengeti Soccer Bonanza.
Katika Bonanza hilo lililozishirikisha
Timu nne lilifanyika jana katika viwanja vya Chuo cha Uhasibu Mbeya(TIA)
zikiwmo timu kutoka Baa ya Kalembo ya Sokomatola, Tugelepo ya Mbata na wenyeji
Wanafunzi wa TIA.
Timu ya Salalizya fc ya Mabatini
ilijinyakulia zawadi ya Katoni 8 za Bia aina ya Serengeti baada ya kuishinda
timu ya Wanafunzi wa TIA katika fainali kwa magoli mawili kwa nunge hivyo
TIA kuibuka mshindi wa pili na kujinyakulia Katoni 4 za bia.
Awali timu ya Salalizya iliifunga
Tugelepo goli moja kwa bila katika mchezo wa utangulizi na kasha timu ya TIA
kuitoa timu ya Kalembo kwa mikwaju 9 kwa 8 baada ya muda wa kawaida
kutofungana.
Mshindi wa tatu ilikuwa ni timu kutoka
baa ya Kalembo baada ya kuifunga timu ya Tugelepo kwa mikwaju 4 kwa 2 ya penati
katika kumtafuta mshindi wa tatu kutokana na kutoshana nguvu katika muda wa
kawaida.
Hivyo Mshindi wa tatu alijipatia Katoni
Mbili huku timu ya Tugeleo ikijipatia Katoni Moja kutokana na kuwa mshindi wa
nne na wa mwisho.
Katika Bonanza hilo Mgeni rasmi
aliyegawa zawadi kwa washindi alikuwa ni Mkurugenzi wa Hoteli ya Kimataifa ya
PADZ iliyopo Forest Mpya, Patrick Zambi, ambaye alitoa wito kwa vijana kupenda
michezo na kujikita katika mazoezi ili kuim,arisha afya zao.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment