Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, September 15, 2014

HOT NEWS: MKUU WA WILAYA YA CHUNYA KUYAKAMATA MALORI YATAKAYOLAZA ABIRIA NJIANI .

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro amepiga Marufuku malori kuwalaza abiria katika magari barabara kutoka namkukwe kwemda Mbeya na Isangawana kwenda Mbeya .

Ameyasema hayo wakati wa Ziara ya kukagua ujenzi wa Mahabara katika Kata 20 za Wilaya ya Chunya baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa Namkukwe na Isanzu ambao wamedai kwamba magari huanza safari saa kumi na mbili jioni na kupumzika katika kituo cha malangali kwa zaidi ya masaa saba huku abiria wakiwa katika malori hayo.

Amewaagiza maaskari kuyakamata magari yote yatakayokaidi Amri hiyo kutokana na adha kubwa wanayopata wasafiri wanaotumia malori hayo.

Na Ezekiel Kamanga

Mbeya yetu

No comments: