Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, August 8, 2014

MKUU WA MKOA WA MBEYA MH. ABBAS KANDORO ATEMBELEA BANDA LA MBEYA YETU BLOG NA KUWAPONGEZA KWA KAZI NZURI WANAYO IFANYA.

Mkuu wa Mkowa  wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro wa kwanza kulia akipata maelezo kutoka katika Banda la Mbeya ambapo alipata Taarifa fupi kuhusu Blog ya Mbeya yetu kutoka kwa Mtaalam wa Mitandao kutoka Tone Multimedia Group Fredy Anthony Njeje kwa Niaba ya Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu Joseph Mwaisango
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro wa kwanza Kulia akifurahi Baada ya kuona Tukio zima la Ziara yake likiwa Live moja kwa moja katika Mtandao wa  Mbeya yetu, Kulia ni Mtaalam wa Mitandao kutoka Tone Multimedia Group wamiliki wa Mbeya yetu Blog akimweleza Mkuu wa Mkoa Jinsi Tukio lilivyo weza kwenda hewani moja kwa moja na kujionea jinsi Mbeya yetu walivyo na Teknolojia kubwa katika mawasiliano 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Abbas Kandoro akitahamaki wakati anaoneshwa tukio la Ziara yake
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro wa Kwanza kushoto Akitoa Mkono wa Pongezi kwa Mtaalam wa Mitandao kutoka Tone Multimedia Group Fredy Anthony kwa niaba ya Mbeya yetu  kwa kuwa wabunifu na kuendana na Dunia ya sasa kwamba mitandao ya kijamii inamanufaa sana kwa Jamii.
Mh. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiendelea kutoa Pongezi zake ndani ya Banda la Mbeya yetu nane nane
Mh. Abbas Kandoro Mkuu wa Mkoa wa Mbeya wa kwanza kulia akiagana na Mtaalam wa Mitandao ya kijamii kutoka Tone Multimedia Group ambao ni wamiliki wa mtandao wa Mbeya yetu  Fredy Anthony Njeje kwa Maelezo mazuri aliyoyapata katika Banda hilo.

Picha zote na Mbeya yetu

No comments: