Hiki ni kipande kifupi sana cha barabara ambacho hakina hata Robo Kilometa , kipande hiki cha barabara ni Muhimu sana kwa sababu Magari ya Mahakama Kuu yanapita hapa, Mahabusu wanapopelekwa Mahakamani wanapitishwa hapa, RPC anapita hapa, Majaji wanapita hapa, Wanasheria wa Serikali wanapita hapa, Benki kuu wanapita hapa, wanafunzi na wananchi wanapita hapa. Lakini cha kushangaza na kustaabisha zaidi kakipande haka ka Barabara kamesahaulika kabisa hakuna anayekitazama ni miaka kadhaa imepita hakuna ukarabati wowote.
Kwa wahusika wa Miundo Mbinu ya Barabara Jiji la Mbeya hivi Kero hii mnaiona
Hiki ni kilima ambapo Mbele jengo kubwa la Ghorofa ni Mahakama Kuu kanda ya nyanda za juu kusini , hapo hapo ndipo unaelekea Benki kuu na Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Lakini Barabara ndio kama inavyo onekana.
Hili ni Moja ya Korongo kubwa ambalo lipo katika kipande hicho cha barabara Hapa pana Afadhali kidogo
Haka kasehemu kamechimbika
Hapa hakuna hata pakukwepea
Hakuna unafuu eneo hili
Makorongo mwanzo mwisho
Magari yanapishana kwa Shida.
USHAURI KUTOKA MBEYA YETU, WAKATI JIJI WANAENDELEA KUJIPANGA KATIKA HILI BASI CHUO CHA MAFUNZO MAGEREZA KAMA KUNA WAKANDARASI WASAIDIE BASI HATA KUWEKA KIFUSI HAPO.
Picha zote na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment