Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, August 29, 2014

KERO ZA BARABARA: MBEYA YETU YAMULIKIA BARABARA YA VETA , AMBAPO KUNA VIONGOZI WA KUBWA WA SERIKALI WANAISHI HUKO PAMOJA NA CHUO CHA MAFUNZO YA UFUNDI STADI VETA.

Hii ni moja ya Kero ya kakipande kadogo sana na korofi ambako wananchi wanaoishi eneo hili wamelalamika sana na kudai kuwa hakuna anayesaidia kwa njia zozote..

Mbeya yetu baada ya kupata taarifa hizo iliona ni vema na haki kutembelea eneo hilo na kujionea wenyewe ambapo mpaka sasa wenye magari wamelazimika kuikimbia barabara hiyo kutokana na kuchakaa vibaya kwa njia hiyo

hata hivyo baadhi ya wakazi wamelalamika sana kuwa njia hiyo hasa hako kakipande kadogo kamekuwa kero kubwa na kusababisha hata mataili yao ya magari kuharibika, kuisha na kuyabadilisha kila wakati
Pia Mbeya yetu ilibaini wazi kuwa kuna Chuo cha ufundi stadi cha veta na hii ikiwa ni moja ya njia kuu na ambapo katika Chuo hicho kuna zaidi ya wanafunzi Elfu mbili sasa swali likaja je hawa wanafunzi hakuna waliosomea Fani ya ukandarasi hata waje kumwaga kifusi na kuziba mashimo hayo?

Na kubwa zaidi katika eneo la barabara hiyo kuna viongozi wakubwa wa Serikali wanaishi huko akiwemo Mkuu wa Majeshi Tanzania, Waziri Asiye na Wizara Maalum, Aliyekuwa naibu Waziri wa Elimu, Viongozi wa  wa Mkoa, Pamoja na Watu wenye uwezo na Baadhi yao pia wameikimbia barabara hii.

Zifuatazo ni picha za  Baadhi ya maeneo ambayo Tochi yetu imemulikia kwa umakini.

 Hiki ndicho kipande cha barabara hiyo ambapo ndipo inapoanzia kwa kutazama unaweza ukasema ni salama lakini ukiangalia kulia kwako utagundua kama kuna shimo lililofunikwa na udongo, Eneo hilo ni mashimo ukipita vibaya unaweza acha tairi zako za Gari
 Haya ni Mawe yaliyochongoka , wengi wamepatwa na pancha katika eneo hili na kusababisha wahame njia hiyo hata kama wanaishi jirani na maeneo hayo.
 Eneo hili ni kucheza Sindimba tuu
 Hakuna Unafuu hata kidogo
 Kwanza kabisa kwa vumbi hili hapa ni hatari sana pia barabara kipande hiki inazidi kuwa mbaya zaidi 
 Hapa huwezi hata kwepa ni lazima utapita tuu na kupita kwake lazima utasababisha majanga na chombo chako cha usafiri


SWALI ... JIJI MPO? JE MMEKUONA NA HUKO.. KAMA BADO PITIENI MTAZAME

PICHA NA MBEYA YETU2 comments:

Anonymous said...

pongezi kwenu kwakufanya kazi nzuri ambazo zinaweza leta maendeleo katika jiji letu

Sir Silvester said...

kuhusiana na hiyo barabara ya VETA mimi nirijaribu hata kumuandikia E-mail bwana sugu kutaka kujua kauli ya serikali lakini nasikitika kua majibu sijapata mpaka leo sijajua labda hakuipata au wingi wa kazi umemfanya ashindwe kuijibu. kwakweli mvua ikinyesha gari ndogo hasa zisizovuta mbele na nyuma haziwezi kupanda hapo kwa usalama