TIMU ya soka ya Waendesha pikipiki
maarufu kwa jina la Bodaboda ya Uyole imeibuka kidedea katika fainali ya Kombe
la Bodaboda dhidi ya timu ya Kabwe katika kipute kilichopigwa juzi katika
uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge Soweto jijini Mbeya.
Katika fainali hizo ambazo zimedhaminiwa
na Kampuni ya vinywaji baridi ya Cocacola Kwanza Mbeya, Mgeni rasmi alikuwa ni
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harisson Mwakyembe aliyekabidhi zawadi mbali mbali kwa
washindi.
Timu ya Uyole aliibuka kidedea baada ya
kuwafunga timu ya Kabwe kwa magoli mawili kwa nunge magoli yaliyopatikana
kupitia kwa Miraji Juma aliyefunga goli dakika ya 41 kipindi cha Kwanza baada
ya piga ni kupige katika lango la Kabwe.
Baraka Agogo aliandikia goli la pili na
la ushindi timu yake ya Uyole baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa timu ya Kabwe
dakika ya 75 na kufanya hadi mwisho wa mchezo Uyole 2 na Kabwe 0 katika
mpambano ulioamuliwa na Mwamuzi Ngole Mwangole.
Awali katika mchezo wa kumtafuta mshindi
wa tatu ulizikutanisha timu za Soweto na Iyunga ambapo timu ya Iyunga
ilijinyakuliwa nafasi ya Msindi wa tatu baada ya kuifunga timu ya Soweto magoli
matatu kwa bila.
Magoli ya timu ya Iyunga yalifungwa na
Salim Mvungi dakika ya 30, na magoli mawili yakifungwa na mshambuliaji hatari
Pinto Iman katika dakika za 70 na 76 na kuwaacha wapinzani wao wakiishia katika
nafasi ya nne hadi kipenga cha mwisho kilichopulizwa na mwamuzi Kefa Kayombo.
Ligi hiyo iliyoandaliwa na kampuni ya
City Sign Promotion & marketing Agency ya jijini Mbeya ilianza kutimua
vumbi Juni 14, Mwaka huu baada ya kufunguliwa na Waziri Mwakyembe kabla ya
kuifunga tena Julai 26, Mwaka huu.
Dk. Mwakyembe alikabidhi zawadi kwa
washindi ambapo mshindi wa Kwanza ambao ni timu ya Uyole alikabidhiwa Kombe
pamoja na mfano wa Hundi yenye thamani ya shilingi Milion mbili kwa ajili ya
ununuzi wa Pikipiki mpya aina ya Boxer, pamoja na mpira mmoja.
Mshindi wa pili timu ya Kabwe
ilikabidhiwa mfano wa Hundi yenye thamani ya shilingi lai saba(700,000) pamoja
na mpira mmoja huku mshindi wa tatu timu ya Iyunga ikikabidhiwa mfano wa hundi
yenye thamani ya shilingi Laki tatu(300,000) pamoja na mpira mmoja huku mshindi
wa nne timu ya Soweto ikiambulia mpira mmoja.
Aidha Dk. Mwakyembe pia alikabidhi
zawadi kwa mfungaji bora ambaye alikuwa ni Emanuel Luole kutoka Timu ya Stendi
ya Umalila Mbalizi aliyejinyakuliwa mfano ya hundi ya shilingi laki moja baada
ya kufikisha magoli saba, Goli kipa bora alitoka tiku ya Kabwe Zakaria Lugano
aliyepata Shilingi Laki Moja pamoja na timu yenye nidhamu ambayo ni Ilomba
iliyojipatia shilingi laki moja.
Hata hivyo Waziri Mwakyembe baada ya
kumaliza kukabidhi zawadi zilizotolewa na wadhamni ambao ni Kampuni ya Cocacola
pia alijitolea zawadi kwa ajili ya mwamuzi bora na mshika kibendera bora ambao
aliwapa shilingi laki moja kila mmoja.
Wakati huo huo Waziri Mwakyembe
alitimiza ahadi yake kwa chama cha Waendesha bodaboda Mkoa wa Mbeya kwa
kuwakabidhi pikipiki mbili mpya pamoja na jezi mbili za mpira wa miguu kwa
ajili ya timu ya jiji itayoundwa baada ya kumaliza ligi hiyo.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment